![]() |
PHOTO PROFILE: Mfano wa madhara yatokanayo na
tetemeko la aridhi.
|
Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.7 kwenye vipimo vya Richter limeikumba eneo la ziwa Tanganyika majira ya saa tisa na dakika thelathini na mbili usiku kuamkia leo, tetemeko hilo lilitikisa maeneo ya kaskazini mwa Zambia na mitetemo yake kufika maeneo ya kusini magharibi mwa mwa mkoa wa Rukwa.
Kwa
mujibu wa shirika la Utafiti wa Jiolojia la nchini Marekani linasema kitovu
chake kilikuwa kilomita 10 chini ya ardhi, umbali wa takribani kilomita 45
mashariki mwa mji wa Kaputa nchini Zambia, mji huo unapatikana katika mpaka wa Zambia
na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Tetemeko
la ardhi lenye ukubwa kama huo huchukuliwa kuwa la kawaida, lakini wataalamu wanasema
kutokana na kitovu chake kuwa chini sana ndani ya ardhi, huenda hilo
lilisababisha mtikisiko kuwa mikubwa.
![]() |
Jiolojia
image: Jinsi
tetemeko linavyoanza chini ya ardhi.
|
Source: bbc swahili


Post a Comment