0
Robin Rhodes mwenye umri wa miaka 57 anatuhumiwa kwa kusema Trump .... atawafukuza nyinyi nyote na baadaye akamzuia mwanamke huyo kutoondoka katika afisi yake.
Profile Photo: Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa John F. Kendedy.

MAREKANI.
Mtu mmoja katika jimbo la Masachussets nchini Marekani ameshtakiwa kwa tuhuma za kutekeleza uhalifu wa chuki baada ya kumpiga teke mfanyakazi Muislamu katika uwanja wa ndege wa John F. Kennedy pamoja na kumkaripia.
Robin Rhodes mwenye umri wa miaka 57 anatuhumiwa kwa kusema Trump ....atawafukuza nyinyi nyote na baadaye akamzuia mwanamke huyo kutoondoka katika afisi yake.
Kushambulia na kuwazuilia watu ni miongoni mwa mashtaka ya uhalifu wa chuki ambao mtu huyo kwa sasa anakabiliwa nayo, pia atakabiliwa na kifungo cha miaka 4 jela iwapo atapatikana na hatia kulingana na hakimu wa mahakama katika Wilaya ya Queens, Pia ameshtakiwa kwa kupiga kelele.
Mfanyakazi huyo wa kampuni ya ndege ya Delta Airlines ambaye alikuwa amevaa hijab alikuwa ameketi katika afisi yake siku ya Jumatano wakati Rhodes alipodaiwa kwenda katika mlango wake na kuanza kumkaripia, kugonga mlango, kumzuia kuondoka na kumpiga teke.
Wakati mtu mwengine alipoingilia kati na kumsaidia mwanamke huyo kutoka ofisini kwake, mtu huyo alidaiwa kumfuata na kupiga magoti mbele yake akiigiza maombi ya kiislamu. ''Islam na Isis, sasa Trump amewasili, atawafurusha nyotea, unaweza kuuliza Ujerumani, Ubelgiji na Ufaransa kuhusu watu hao utaona kilichojiri''.


Source BBC


Post a Comment

 
Top