0
Tamasha la utalii na kupiga vita ujangiri, tembelea mbuga zetu limekusanya jumuiya za waandishi pamoja na wadau wa sekta ya utalii katika jiji la Arusha huku kukiwepo na mada mbalimbali zinazogusia changamoto za utalii, sheria za kiuandishi, ujangiri pamoja na uandishi wa habari za utalii ambapo tamasha hilo limeanza kwa kuwepo kwa mijadara kadhaa.

Katibu wa vyama vya waongoza watalii nchini Emmanuel Mollel azungumzia changamaoto kadhaa zinazowakabili kwa upande wao.

Wadau wa sekta ya utalii na wana habari wakifuatilia majadiliano wakati wa Arusha Tourism Festival (conference) iliyofanyika mapema leo jijini Arusha

Loshee Mollel kiongozi wa wapagazi akizungumza juu ya kazi wanazozifanya wasaidizi wa watalii wawapo katika kazi zao.


Afisa utalii wa mkoa wa Arusha Flora akielezea namna serikali inavyowakilishwa katika jamii ambapo raia yeyote ana nafasi katika maendeleo ya nchi, kulia kwake ni wadau wa sekta ya utalii.


Waandishi wa habari na wadau wakiwa katika picha ya kundi wakati wa mijadara ya tamasaha la utalii na wana habari jijini Arusha.

Waandishi wa habari na wadau wa sekta ya utalii wakiwa katika mkutano wa mijadala kuelekea kwenye Tamasha la Utalii Arusha.

Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri mkoani Arusha Claudi John akitoa mchango kuhusu changamoto za sekta ya utalii pamoja na waandishi wa habari.

Neville Meena mwenyekiti wa jukwaa la wahariri nchini akitoa semina kwa wadau wa utalii na waandishi wa habari katika hoteli ya Palace Hotel.




ARUSHA.
Wakizungumza katika majadiliano yaliyofanyika siku moja kabla ya tamasha litakalofanyika kesho katika uwanja wa sheikh Amri Abeid jijini Arusha katibu wa vyama vya waongoza watalii nchini Emmanuel Mollel amesema waongoza watalii wanapata wana changamoto zinazowakabili zikiwemo kuhitaji, marekebisho ya sheria ya ulipaji wa ada.

Uwepo wa vyuo vinavyostahili kutoa elimu mahususi pamoja na kutambulika kimataifa, hii ni kutokana na vyuo vilivyopo bado havitambuliki kimataifa nafasi inayofanya kukosa nafasi za kazi nje ya mipaka, pamoja na hilo tozo zinazotozwa kwa makampuni yanayopeleka watalii polini.

Hata hivyoUharibifu wa mazingira unaotokana na tabia nchi,umeonekana nayo kuleta madhara katika sekta ya utalii nchini hii inaweza kuepushwa enadpo nafasi ya utoaji elimu kwa watu wanaoishi pembezoni mwa maeneo ya mbuga bado inanafasi kwa wananchi hao ili waweze kuyatunza.

Vilevile Ujangiri, unaharibu sifa nzuri ya nchi yetu hali hii inawafanya wanaopeleka watalii kwenda kuangalia wanyama  kuona haibu kutokana na baadhi ya wanyama kutokuwepo na kutoweka.

Naye wadau wa sekta ya utalii wakiwemo wapagazi waliowakilishwa na katibu wao Leshee Mollel ambaye ameeleza kuhusiana na kitengo chao kinavyokumbana na matatizo mbalimbali ikiwemo kutopata haki zao za msingi ikiwemo mishahara.

Katibu wa Wapagazi; mara kadhaa wamekuwa watu wanaobeba mizigo ya watalii kuelekea sehemu mbalimbali za kitalii mfano kubeba mabegi yenye uzito unaokadiriwa mpaka kufikia kilo 30 na kupanda nao mlima Kilimanjaro. Kazi ya kubeba mizigo ya watalii ni nzito sana maana magari hayawezi kufika.


WAJIBU WA VYOMBO VYA HABARI KATIKA SEKTA YA UTALII:

Mwenyekiti wa jukwaa la wahiriri nchini Nevile meena, amezungumzia mambo kadhaa huku akigusia majukumu ya uandishi wa habari katika kuwakilisha habari kwa umma, kuanzia upatikanaji, mtu wa kwanza kutoa habari ni mwandishi mwenyewe, wakati chombo cha habari kinasimama katika muhimli wa nne wa sheria katika nchi bado mwandishi ana nafasi kubwa kuelemisha na kupeleka habari kwa jamii huku ndiye mtu mwenye ukaribu wa mwananchi.


“Bahati mbaya mwandishi wa habari wa nchini anapenda kuajiliwa kutokana na  malipo tofauti na mwandishi aliye nchi za ulaya ambaye yeye anapewa malipo makubwa kama ni mwandishi binafsi, vilevile mwandishi anapaswa kuwa wa kwanza kufaham iwe mvua hama jua na kwa mazingira yoyote kupata habari”Alisema Meena.

Post a Comment

 
Top