Chanjo hizo ni zile ambazo huwa zinatolewa kwa watu wanasafiri nje ya nchi kama kinga kwa ajili ya homa manjano.
![]() |
| Profile Photo. |
DAR
ES SALAAM.
WATU
saba, akiwamo mmoja anayedaiwa kuwa daktari bandia, wanashikiliwa na Jeshi la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa madai ya kutengeneza kadi bandia za
chanjo ya homa ya manjano na kuziuza kwa watu wanaofika hospitali ya Mnazi
Mmoja kwa ajili ya kupata huduma hiyo.
Kamishna
wa Kanda hiyo, Simon Sirro, akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam, alimtaja aliyejifanya daktari kuwa ni mfanyabiashara Salum Natali (47),
mkazi wa Chanika Magengeni, aliwataja watuhumiwa wengine ni walinzi watatu
ambao ni Aisha Hassan (29) mkazi wa Vingunguti Mikoroshini, Yakobo Msenga (42)
mkazi wa Chanika na Junith Dunstan (23) mkazi wa Kiwalani.
Wengine
ni Oliver Bwegege (58) mkazi wa Kigogo Mkwajuni, mjasiriamali Fredy Nyomeye
(44) mkazi wa Chang’ombe na fundi umeme Mohamed Bwanga (59) mkazi wa Majohe
Gongo la Mboto.
Alisema
watu hao walikamatwa Januari 16, mwaka huu majira ya saa 11:00 asubuhi baada ya
mtoa taarifa (jina linahifadhiwa) kufika hospitalini hapo na kutakiwa kutoa
fedha na mmoja wa watuhumiwa hao ili kupatiwa kadi hiyo ya chanjo ya homa ya
manjano.
Katika
mahojiano, watuhumiwa hao walikiri kufanya kosa hilo la kughushi na kutoa kadi
hizo za chanjo pasi na mtu kuchomwa sindano yenyewe ya chanjo, alisema.
Kamishna
Sirro alisema Natali alikuwa akijifanya kuwa ni daktari aliyekuwa akiwachoma
watu sindano, aliongeza kuwa uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea ili
kuwabaini washiriki wengine katika mtandao huo wa utoaji wa kadi hizo bandia za
chanjo bila kutoa chanjo yenyewe husika.
Source NIPASHE.

Post a Comment