Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Charels Tizeba akiwaeleza wanahabari (Hawapo Pichani) athari za uvuvi haramu na jinsi unavyoathiri uchumi wa nchi. |
DAR ES SALAAM
Serikali imewaagiza
wakurugenzi nchini hasa kwenye maeneo wanayojishughulisha na uvuvi kuwachukulia
hatua maafisa uvuvi wanaoshindwa kutimiza wajibu kwa kushindwa kuzuia uvuvi
haramu.
Akizungumza mara
baada ya kumalizika kikao cha kamati kilichohusisha Wizara saba Maliasili,
Ulinzi, Nishati na Madini Tamisemi, Kilimo, Mifugo na Uvivi pamoja na Mambo ya
Ndani Naibu Waziri TAMISEMI Suleiman Jaffo aliwataka watendaji hao kutumia
agenda ya kupambana na uvuvi haramu kuwa agenda ya kudumu katika vikao vyao.
Alisema kuwa
maofisa uvuvi hao wanatakiwa kupimwa wajibu na utendaji kazi zao kwa kuangalia ni
kiasi gani wanajihusisha na masuala mazima ya kupambana na uvuvi wa kutumia
mabomu. “Kuna baadhi ya
mafisa uvuvi wanahusika na vitendo vya uvuvi haramu nchini hivyo kuanzia kesho
wataanza kupimwa wajibu wao na kwa atakayeshindwa kutimiza wajibu atatolewa
katika nyazifa hiyo”.
Kwa upande wake
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Januari Makamba alisema kuwa nchi yetu
inaeneo kubwa la bahari na kwa miaka kadhaa nchi yetu imekuwa na changamoto ya
uvuvi haramu, hivyo tumeona kuna haja ya kuchukua hatua ya haraka katika
kupambana na uharamia huo.
Akifafanua zaidi
kuhusu hilo Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Charels Tizeba alisema kuwa jambo
la uvuvi haramu lisipochukuliwa kwa umakini litapelekea kuathiri uchumi wa nchi
hivyo lengo la Serikali ni kukomesha uharibifu unaojitokeza sasa. Aliemdelea kusema kuwa ni aibu kwa
taifa letu kuendelea kuvua kwa njia haramu kwani nchi nyingi kwa
sasa zimeondoka katika uvuvi wa namna hiyo.
Naye Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba alitoa wito kwa watanzania wote
kushirikiana na Serikali katika kufichuwa wale wanaohusika na uvuvi haramu, pia alisisitiza kuwa “kila mtanzania anawajibu wa kuwa makini katika kulinda
rasilimali za majini tulizo nazo”.
Kikao hicho ni
utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais la kupambana na uvuvi haramu ambapo maazimio
hayo yatafanyiwa kazi na kuahidi kukutana baada ya miezi sita kwa ajili ya
kutafakari hatua zilizochukuliwa pamoja na kurekebisha pale patakapoonekana
pana changamoto.
Post a Comment