Mwenyekiti anayemaliza muda wake Imani Matabula
akiongea na wanashirikisho wa vyuo vikuu hawapi pichani pamoja na kuwaaga kutokana na kumaliza muda wake. |
Wajumbe wa mkutano mkuu wa shirikisho la vyuo
vikuu wakiwa tayari kufanya uchaguzi kuwachagu viongozi wao wapya kwa kipindi kipya. |
Mwenyekiti wa Shirikisho la vyuo vikuu mkoa wa
Dar Es Salaam Iman Matabula (kulia) Mganwa Mzebwa –Katibu Hamasa shirikisho vyuo vikuu Taifa na Debora Charles Katibu msaidizi wa shirikisho |
Baadhi wa wajumbe wakisikiliza ahadi za mmoja wa
wagombea (hayupo pichani) mkutano mkuu wa shirikisho la vyuo vikuu wakiwa tayari kufanya uchaguzi kuwachagua viongozi wao wapya kwa kipindi kingine. |
DAR ES SALAAM
Mkutano mkuu wa
wanachama wa ccm shirikisho la vyuo
vikuu nchini mkoa wa Dar es salaam unafanya uchaguzi wa kuwachagua viongozi wa shirikisho leo
jijini Dar es salaam mara baada ya
viongozi wanaomaliza muda wao wa uongozi wa mwaka mmoja kumalizika.
Akiongea na
wajumbe wa chama cha mapinduzi katika mkutano huo wa kuwachagua viongozi wapya
mwenyekiti wa shirikisho anaemaliza muda wake Bw. Imani Matabula amesema kama
kiongozi ni vema kuwa mstahimilivu katika kila jambo kwakuwa uongozi ni
utumishi hivyo ni lazima kukubali kukosolewa ili kujenga nafasi ya uongozi
bora.
Ameongeza kuwa ni vema
kiongozi kuwa na nidhamu kwa wananchi, kuwaheshimu na kuwajali kwa misingi ya katiba na kuwataka
wajumbe wa shirikisho kuwapima wagombea wanaowania nafasi hizo kwa uwezo wao, hekima na mikakati waliyonayo.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
HABARI BAADA YA UCHAGUZI:
Katika uchaguzi huo uliofanyika jana kwa
wagombea kuomba kura kutokana nafasi zao, ulichukua muda wa masaa mengi mpaka kukamilika
kwake ambapo mpaka kufika saa 2200 usiku ndipo majina kura zilitangazwa na
kupatikana kwa viongozi watakaoendeleza kurudumu la kiungozi kwa kipindi
kijacho.
Jumla ya wagombea zaidi ya kumi na nafasi
zilizokuwa zinahitajika ni tano, Mwenyekiti, Katibu, Katibu mwenezi, Katibu
uchumi na fedha na Ktibu hamasa ambapo katika nafasi hizo walioshinda nagfasi
hizo ni kama ifuatavyo;
1.
Fredrick
Ludovic –Mwenyekiti Seneti Mkoa.
2.
Rahma
Hassan –Katibu Seneti Mkoa.
3.
Kihaka
Adam –Katibu Mwenezi Seneti Mkoa.
4.
Evance
Kirumbi –Katibu Uchumi na Fedha.
5.
Yassin
O. Makaraba –Katibu Hamasa.
Post a Comment