Photo Profile: Mfano wa kisu ila hakihusiki. |
Baadhi ya ndugu wa jamaa waliokatwa vichw wakiwa
katika majonzi. |
Wanachama na wahalifu wa magenge tofauti huzuiliwa katika magereza tofauti nchini Brazil |
Genge moja la uhalifu linaloendesha shughuli zake katika magereza mbalimbali nchini Brazil, limewakata vichwa takriban wafungwa 33 katika gereza moja kwenye jimbo lililopo Kaskazini la Roraima.
Ni tukio la pili chini ya juma moja kutokea nchini
Brazil, ambapo maofisa wa Serikali wanaamini kuwa kukatwa vichwa huko kunatokana
na mzozano unaondelea miongoni mwa wanachama wa genge hilo lijulikanalo kama
PCC.
Gereza hilo
lililosongamana liko eneo la mashambani, nje ya mji mkuu wa jimbo wa Boa Vista
na hadi kufikia sasa maiti 31 zimepatikana na nyingi ya maiti hizo zimekatwa vichwa
au kukatwakatwa vipande.
Maofisa wa
Serikali wanasema ghasia hizo ni sehemu ya juhudi za magenge kuwa na mamlaka
katika baadhi ya magereza.
Post a Comment