Mindi
Kasiga –Wizara ya mambo ya nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na kimataifa kutoka kitengo cha mawasiliano. |
DAR ES SALAAM.
Mpango
wa taifa wa maendeleo wa mwaka 2016-2020 na ahadi za serikali ya rais Magufuri
katika kipindi chake ni kuwa na uchumi wa viwanda, waziri wa mambo ya nje wa
china Mh. Wang Yi anatarajiwa kuufanya ziara ya kikaziya siku moja hapa nchini
mnamo Januari 09.2017 ambapo atapokelewa na mwenyeji wake waziri wa mamabo ya
nje Balozi Dtr Augustine Maige.
.
Madhumuni
ya ziara hiyo ikiwa ni kukuza mahusiano ya kihistoria kati ya nchi hizi mbili
Tanzania na china uliodumu zaidi ya mika hamsini, hata hivyo mh. Wang Yi atafanya
mazungumzo na mwenyeji wake Dtr Maiga kuhusu ushirikiano wan chi hizi mbili pia
waziri huyo wa china atakutana na Rais Magufuri kwa lengo la kumsalimia.
Desemba
2015 itakumbukwa kuwa mkutano wa wakuu wa nchi za afrika na china china
iliichagua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi nne za afrika zitakazowezeshwa
kupiga hatua kwenye maendeleo ya viwanda, mbali na mradi mkubwa wa ujenzi wa
viwanda 200 unaoendana na mpango wa serikali wa viwanda vinavyotarajiwa
kuwekezwa kwa kujengwa hapa nchini kabla ya 2020, China imeahidi kuisaidia Tanzania
kuboresha Reli ya TAZARA, Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo pamoja na ujenzi wa
Reli ya kati.
Masuala
ya Amani na usalama katika eneo la Afrika masahariki yatazungumziwa kwa kina
pamoja na mawaziri hao wawili watagusia nyanja ya kimataifa ikiwa ni pamoja na
mageuzi ya Balaza la Usalama LA Umoja wa Mataifa, ambapo china inaunga mkono
msimamo wa Afrika na wa Tanzania wa kutaka Afrika ipewe viti viwili vya kudumu
katika balaza hilo.
Post a Comment