 |
Profile Photo: Zanzibari Mji Mkongwe unavyoonekana ukiwa kwenye chombo baharini. |
 |
Profile photo: Lowassa kushoto na Maalim Seif kulia. |
ZANZIBAR..
Wanasiasa wakongwe
nchini, Maalim Seif Sharif Hamad aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
na Edward Lowassa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
katika, kesho wanatarajia kuungana kwa mara ya kwanza jukwaani tangu kumalizika
kwa uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Vigogo hao wa vyama
vya CUF (Maalim Seif) na Chadema (Lowassa) wataunguruma katika viwanja vya
Skuli ya Fuoni visiwani Zanzibar kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Dimani kwa
tiketi ya CUF, Abdulrazaq Khatib Ramadhani, katika uchaguzi mdogo utakaofanyika
Januri 22 kuziba nafasi ya aliyekua mbunge wa jimbo hilo, Hafidh Ally Tahir
aliyefariki dunia Novemba 11 mwaka jana.
Naibu Katibu Mkuu
wa Chadema, Salum Mwalimu amesema kuwa chama chake kimemua kuungana na CUF
katika uchaguzi huo ili kuhakikisha mshirika wake huyo wa Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) anamshinda mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Aidha, Mwalimu
aliongeza kuwa baada ya Lowassa kushiriki uzinduzi wa kampeni hizo kesho,
viongozi wengine wa Chadema watafuata kwa kufanya mikutano mbalimbali jimboni
humo. Alisema kuwa baada ya Lowassa atafuata Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman
Mbowe pamoja Tundu Lissu kwa nyakati tofauti, kisha wengine wataendelea hadi
mwisho wa kampeni hizo.
Akizungumzia uamuzi
huo wa Chadema, Mkurugenzi wa Habari,Uenezi na Mawasiliano kwa Umma, Salim
Bimani alieleza kufurahishwa na uamuzi huo wa Chadema na kueleza kuwa hatua ya
Lowassa kuhudhuria uzinduzi huo itaongeza hamasa kubwa kwa wapenzi wa chama
hicho.
“Umenambia hadi
Lowassa atakuwepo? Ni furaha iliyoje, Wanzibari wana shauku kumuona. Siku ya
kampeni patakuwa hapatoshi Skuli ya Fuoni, hapa Simba (Maalim Seif) kule
Lowassa kipenzi kingine cha Wazanzibar,” Bimani anakaririwa na Mwananchi.
Aliongeza kuwa kama
Lowassa atahudhuria mkutano huo atakuwa na mambo mawili makubwa ya kufanya, la
kwanza likiwa kuwashukuru Wazanzibar kwa kura walizompa katika uchaguzi Mkuu wa
mwaka jana. Na la pili litakuwa kumpigia kampeni mgombea wa CUF, Abdulrazaq
Khatib Ramadhani.
Lowassa ambaye ni
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Maalim Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF,
wataingia katika jimbo hilo ikiwa ni siku chache baada ya Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana kufanya uzinduzi wa kampeni hizo akiambatana na viongozi
wengine wa kitaifa wa chama hicho.
Hivyo, kwa muktadha wa kisiasa, vigogo hao wa
Ukawa wana kazi ya kusawazisha matuta yaliyowekwa na timu ya chama tawala
iliyoongozwa na katibu mkuu wa ccm Kinana.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.