Mh. Samia Suruhu akitoa hotuba kwenye mkutano wa nane wa
majaji wanawake nchini.
|
DAR ES SALAAM
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaagiza majaji na
mahakimu wanawake kote nchini kupambana ipasavyo katika kukabiliana vitendo vya
rushwa, unyanyasaji wa kijinsia pamoja na rushwa ya ngono ili kusaidia wanawake
kupata haki zao za msingi bila kubaguliwa katika jamii.
Mh. Samia ametoa
agizo hilo wakati anafungua Mkutano mkuu wa nane wa Chama cha Majaji na
Mahakimu wanawake Tanzania (TAWJA) jijini Dar Es Salaam mapema leo, pia ameonya
kuhusu vitendo vya rushwa ya ngono inayofanywa na baadhi ya watendaji wenye madaraka
na kusema tabia hiyo mbaya ni lazima ikomeshwa mara moja katika jamii.
Ameongeza kuwa
kitendo hicho huzuia na kukwamisha juhudi za wanawake kufikia huduma za kijamii
na za kiserikali ipasavyo ikiwemo elimu, ajira na haki kwa ajili ya ustawi wa
wanawake.
Aidha Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan amekishukuru Chama cha Dunia cha Majaji Wanawake
(IAWJ) kwa mchango na msaada wake kwa TAWJA katika programu ya miaka mitatu ya
kupambana na matumizi mabaya ya madaraka na rushwa ya ngono.
Makamu wa Rais pia
ameipongeza wizara ya Katiba na Sheria, Shirika la UN Women na wadau wengine wa
TAWJA kwa kuunga mkono mapambano ya aina zote za ubaguzi na ukatili dhidi ya
wanawake na watoto nchini.
Amesema elimu ya
haki za Binadamu iliyotolewa na Chama hicho imeleta badiliko kwa wengi kwa njia
ya mafunzo na machapisho, hivyo jitihada lazima ziongezwe ili huduma hiyo iweze
kuwafikia wananchi wengi zaidi kote nchini.
Mh. Samia Suruhu katikati
waliokaa, Jaji mkuu Othman Chande -wa pili kushoto waliokaa, Jaji mkuu wa
Zanzibar kushoto aliyekaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya majaji wanawake
mahakama nchini.
Amesema elimu ya
haki za Binadamu iliyotolewa na Chama hicho imeleta badiliko kwa wengi kwa njia
ya mafunzo na machapisho, hivyo jitihada lazima ziongezwe ili huduma hiyo iweze
kuwafikia wananchi wengi zaidi kote nchini.
Amesisitiza
wanachama wa Chama cha TAWJA waendelee kutoa msaada katika kuwasaidia wanawake
na watoto ambao wanakandamizwa kwa kunyimwa haki zao katika jamii ili waweze
kupata haki zao nchini.
Kwa upande wake,
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mohamed Chande Othman
amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa mkakati wa uimarishaji wa shughuli za
mahakama nchini unaendelea vyema lengo likiwa ni kutenda haki kwa wananchi kote
nchini bila ubaguzi.
Kauli mbiu ya
mkutano mkuu wa nane wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (TAWJA) imekuwa
ni “Kuongoza njia kufikia hitajio la upatikanaji wa
haki kwa wote na kwa wakati”.
Post a Comment