Wabunge wanawake wa upinzani, wametoa wito kwa wanawake wenzao nchini humo, kuwanyima tendo la ndoa waume zao hadi pale watakapojiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi agosti mwaka huu.
Maofisa wa tume huru ya uchaguzi nchini Kenya,
IEBC, wakiwa katika shughuli ya kuandikisha wapiga kura wapya -16 Januari 2017. |
MOMBASA.
Mbunge Mishi Mboko ambaye ameolewa
amesema kuwa wanawake wanapaswa kutofanya tendo la ndoa na waume zao hadi pale
watakapowaonesha vitambulisho vya kupigia kura."Wanawake kama mume wako hatajiandikisha, usimpe unyumba na
mwambie akajiandikishe na kisha arudi nyumbani akiwa na kitambulisho cha
kura," alisema
mbunge huyo.
Wabunge hao wanawake walikuwa
wakizungumza wakati wa kampeni zao za kisiasa kwenye eneo mjini Mombasa,
ikiwa ni sehemu ya kampeni yao kuwahimiza raia kujitokeza kwa wingi na kwenda
kujiandikisha tayari kwa uchaguzi wa mwezi Agosti mwaka huu.
Wabunge hao wamesema kuwa, suala la
ngono ni moja ya silaha kubwa inayoweza kutumiwa na wanawake, kuwashinikiza
waume zao kwenda kujiandikisha ili kufikisha idadi ya wapiga kura watakaofanya
rais Uhuru Kenyatta kuondoka madarakani.
Katika hatua kama hiyo, waendesha
pikipiki maarufu kama bodaboda, nao wamegoma kuwapakia abiria ambao wanashindwa
kuonesha ikiwa wana kitambulisho cha kupigia kura.
Mamlaka zinazohusika na uchaguzi nchini humo zinakadiria kuwa zaidi ya watu
milioni 4 au 6 bado hawajajiandikisha idadi ambayo wadadisi wa mambo wanasema
ni muhimu katika kuamua matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu
Post a Comment