Wakazi wa eneo la Isanga katika jiji la Mbeya wameendelea
kushuhudia visa na mikasa na vioja, baada ya mtoto wa miaka 9 aliyekuwa
amezikwa jana kwenye makaburi ya Isanga kukutwa akiwa kitandani kwake amelala
usingizi mara baada ya kurejea kutoka makaburini.
Profile Photo. |
MBEYA.
Mara baada ya kufika nyumbani familia ikiwa inaingia ndani
nyumbani, walipigwa na butwaa baada ya kukuta mtoto wao amelala kitandani
kwake, na baada ya kuitana na kumwamsha mtoto huyo aliamka na kuonekana
akishangaa hali aliyoiona pale nyumbani.
Kwa pamoja wananchi na wanafamilia walikubaliana asubuhi hii
kwenda kufukua kaburi hilo ili waone nini kilichozikwa, na hivi dakika hizi
zoezi hilo linaendelea na picha za makabuni hapo .
Kaburi lilifukuliwa, hakuna kilichokutwa ndani ya jeneza yaani
maiti iliyozikwa jana haikuwemo, polisi walilazimika kupiga mabomu ili
kutawanya watu pale makaburini baada ya kuanza hali ya sintofahamu juu ya nini
kimetokea?
Kamanda wa Polisi wa Jiji la Mbeya ambaye amatoa maelezo
kuwa, ushahidi wa kimazingira unaonyesha kuwa mwili wa mtoto huyo ulisahaulika
kuwekwa katika sanduku na baada ya ibada mwili haukuagwa.
Baada ya kuzika waliporudi nyumbani ndipo waliukuta mwili wa
mtoto huyo ukiwa umelala kitandani. Jeshi la Polisi liliimarisha ulinzi katika
maeneo hayo ya msiba ambapo amemthibitishia kuwa kaburi limefukuliwa na jeneza
limekutwa likiwa tupu halina kitu.
Inavyoonekana kuna uzembe katika kuandaa mwili na kuuweka
katika jeneza, ingawa pia majirani na watu wanaoishi mazingira hayo wanahusisha
na imani za kishirikina.
Chanzo Mbeya yetu.
Post a Comment