Donald
Trump ameapishwa na kuwa rais wa 45 wa Marekani katika sherehe iliyofanyika
katika majengo makuu ya Bunge la Congress, Washington DC.
MAREKANI.
Baada ya kupigiwa mizinga 21 Donald Trump alitoa hotuba
yake ya kwanza kama rais ambapo ameahidi kuwapa nafasi kubwa wananchi wa Marekani
katika madaraka, akisema wamewasahaulika kwa muda mrefu sana. "Siku hii
ya leo ni yenu na Marekani ni nchi yenu," amesema Trump.
Akiweka mkono wake wa kushoto juu ya Biblia mbili, huku
akiinua mkono wake wa kulia Trump amekula kiapo mbele ya Rais wa Mahakama Kuu
John G. Roberts Jr.
Katika hotuba yake, Donald Trump amesema anajutia
kuona Marekani ilitajirisha nchi za nje kwa gharama za Marekani. Trump amesema. "Tangu
siku hii ya leo, Marekani itapewa kipaumbele sawa na suala la biashara,
viwanda, au uhamiaji", amebaini Bw Trump.
Post a Comment