0
Zifuatazo ni picha tofauti za matukio kadhaa ya mahafari ya 12 ya chuo kikuu cha suza kampasi ya mjini magharibi ambayo mwandishi wa TODAYS NEWS imefanikiwa kuzipata wakati wa mahafari hayo;


Wahitimu wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na waziri wa elimu wakati wa mahafari yao chuoni hapo mapema leo asubuhi.



Rais wa Zanibar na mkuu wa chuo cha suza akimtunuku mmoja wa wahitimu ambaye amefanya vema katika ufaulu wa lugha ya Kiswahili.


Wageni maalum kutoka serikalini na sehemu mbalimbali za Zanzibar ambao walikuwepo kushuhudia kila hatua ya shuguli nzima.

Rais wa Zanzibar (katikati waliokaa) akiwa na makamu mkuu wa chuo na vongozi wengine wa chuo kikuu cha suza katika mnara wa karafuu uliopo chuoni hapo.



ZANZIBAR.
Rais za Zanzibar na mwenyekiti wa balaza la mapinduzi ambaye pia ni mkuu wa chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Dr. Mohamed Shein amewatunuku wahitimu wapatao 861 kutoka vitivo tofauti vya elimu kuanzia ngazi ya cheti, stashahada, shahada na degree katika kampasi ya Tunguu iliyopo mjini Magharibi.

Katika mahafari hayo Dr. Shein amesema walimu wa vyuo vikuu nchini wanajukumu la kuendeleza lugha ya Kiswahili kwa wananfunzi ili kuengeza kasi ya kukuza lugha hiyo kutokana na  kuwa lugha inaendelea kushika kasi na kutambulika katika mataifa kadhaa duniani hivyo ni jambo jema kwa wasomi wa vyuo vikuu kuwa ni miongoni mwa wale watakaokikuza.




Post a Comment

 
Top