Kati
ya benki ambazo zimekuwepo katika utoaji wa huduma hapa ncini Benki ya posta
inafahamika kwa kwa muda mrefu, TPB Bank ilianzishwa mwaka 1925 ambapo mpaka mwaka
1991 iliingia katika mfumo wa kujitegemea na mnamo Machi 23 mwaka jana
ilisajiliwa na kuruhusiwa kutumika kwa jina la TPB Bank PLC.
Nembo ya zamani iliyoagwa kushoto na kulia ni nembo
mpya inayoanza kuitambulisha Bank ya Posta nchini
|
Waziri wa fedha na Uchumi Dr. Philip
Mpango akikaribishwa na wafanyakazi wa benki ya posta katika ukumbi wa
kimataifa wa Mwl. Nyerere.
|
Dr. Mpango akisaini akisaini kitabu cha
wageni.
|
Dr. Mpango akibadilishana mawazo na Dr.
Mpango kabla ya kuzindua nembo mpya.
|
Afisa
mtendaji wa Tpb Bank Sabasaba Moshingi akiongwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa
nembo.
|
Mwenyekiti
wa bodi ya wakurugenzi waTpb Benki Profesa Lettice Rutashobya akielezea safari
ndefu ya benki hiyo mpaka kufikia hapo.
|
Kutoka
kushoto; Peter Mapigano, Bonaventura Paul ambaye ni meneja wa Matawi, Leonira
Kazinja wakimsikiliza mwenyekiti wa bodi ambaye alikuwa akitoa taswira ya benki
toka enzi ya mkoloni.
|
Waziri
wa fedha na Uchumi Dr, Mpango akitoa hotuba iliyosisitia kwa benki hiyo
kujikita kutoa mikopo uenye riba nafuu pamoja na matarajio ya serikali kuona
benki hiyo inawafkiwa watanzania wote.
|
Waziri
wa fedha na Uchumi Dr, Mpango akipiga makofi huku mwenyekiti wa bodi Lettice
Rutashobya akishuhudia kulia.
|
Zawadi ya kukumbuka ambayo Dr, Mpango alikabidhiwa pamoja na saa ya ukutani alikabidhiwa kadi mpya ya benki ambayo ina mwonekano mpya, katikati ni Afisa mtendaji wa Tpb Bank Sabasaba Moshingi. |
Picha
ya pamoja ya watendaji wa benki hiyo wakiwa mbele ya nembo mpya ya utambulisho
wa benki hiyo.
|
DAR
ES SALAAM.
Watanzania wametakiwa kununua hisa
kwa wingi ili kupanua wigo wa kumiliki makampuni ya hapa nchini badala ya kuwachia
wageni.
TPB Bank ilianzishwa mwaka 1925
ambapo mwaka 1991 iliingia katika mfumo wa kujitegemea ambapo Machi 23 mwaka
jana ilisajiliwa na kuruhusiwa kutumika kwa jina la TPB Bank PLC.
Akizungumza
katika uzinduzi wa jina jipya na nembo ya Benki ya Posta (TPB Bank PLC)
uliofanyika jijini Dar es Salaam mapema leo, Waziri wa Fedha na Uchumi Dk.
Philip Mpango amesema watanzania wamekuwa wakilalamika kuhusu umiliki wa
makampuni ya ndani huku wakishindwa kununua hisa na kuwaachia wageni
wakimiminika kwa wingi kununua hisa hizo.
“Naomba watanzania wanunue hisa za TPB Bank,
tujifunze na sisi sasa kushiriki kikamilifu katika soko la hisa na ndio umiliki
wenyewe, tusingoje kuita watu wengine waje kuona umuhimu wa hisa,” alisema Dk. Mpango.
Vile
vile Dk. Mpango amesema watanzania wamekuwa wabunifu hususani wanawake lakini
changamoto kubwa imekuwa mtaji lakini kwa ujio mpya wa TPB Bank changamoto hiyo
itaweza kutatuliwa kwa pamoja huku serikali ikiwepo.
Hata
hivyo alisisitiza kuwa watanzania wanapaswa kujengwa utamaduni wa kujiwekea
fedha za akiba katika mabenki kutokana na maendeleo makubwa ya sekta ya kibenki
nchini ambao utawasaidia kutatua changamoto mbalimbali za kimaisha.
Kwa
upande wake Afisa Mtendaji wa TPB Bank Sabasaba Moshingi amesema mpaka mwaka
2011 kulikuwa na idadi ndogo ya watanzania wanaotumia huduma za kibenki lakini
ubunifu ambao umefanyika kufikia sasa umeongeza matawi ya benki hiyo kutoka 28
hadi kufikia 60 mpaka kufikia sasa.
Aidha
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo Profesa Lettice Rutashobya
alimhakikishia Waziri wa fedha kuwa benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora kwa
wateja wake hususani kwa watanzania walioko pembezoni na hasa vijijini ili nao
waweze kufaidika na huduma zake.
Kindamba
Haule Meneja wa benki ya posta tawi la Mkwepu
akiongea
na mwandishi wa TODAYS NEWS kuhusu
matarajio
anayoyatazamia
mara baada ya uzinduzi wa Tpb Bank.
|
Pamoja
na hayo meneja wa benki hiyo tawi la Mkwepu Kindamba Haule ana matarajio
makubwa kufikia malengo kutokana na mabadiriko wanayofanya katika benki yao
ambapo kwa tukio la ubadirishaji wa nembo ni hatua mojawapo inayofanya wateja
waweze kuona mwanga mpya.
“hatutarajii kubaki palepale kutokana na hatua
hii, maana tumetoka katika hatua ya watu kutunza fedha katika chago na tunaenda
katika kuwafanya wateja watunza fedha ikiwa mkononi mwake kutoka kwetu na
matarajio ni makubwa hata kupitia amana za wateja, pia huduma zetu ni tofauti
na benki nyingine ikiwa ni kutokana na ukomavu wa muda mrefu hapa nchini” alisema Kindamba Haule.
Post a Comment