CUF Flag |
Mwenyekiti wa kamati ya uongozi Julias Mtatiro akiongea na
wanahabari kuhusu kuhamishwa/kutakatishwa kwa fedha za chama cha CUF.
|
Katikati Mwenyekiti wa kamati ya Uongozi Julias Mtatiro (kushoto)
Mbunge viti maalum na Severine Mwaijage (kulia) Kaimu naibu katibu mkuu na
mkurugenzi wa fedha Jaram Bashange
|
DAR ES SALAAM.
Chama cha wananchi –CUF
wafanya mkutano wa wanahabari jijini Dar Es Salaam kuhusu masuala kadhaa
ikiwemo uhamishwaji wa fedha kutoka kwenye akaunti ya chama kwenda kwa akaunti
iliyofunguliwa muda mfupi na watu waliosimamishwa uanachama na wengine si wanachama wa chama hicho.
Fedha hizo zilizotoroshwa kutoka hazina ya serikali kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 05.01.2017 na kuingizwa kwenye akaunti yenye jina sawa na la awali iliyopo NMB tawi la Temeke, imeonekana si akaunti halali kwa mujibu wa wadhamini wa chama cha CUF ambao wamesema hawaitambui akaunti hiyo na haikuwahi kuiidhinisha ipokee ruzuku ya chama hicho.
Akiongea na wanahabari jijini Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa kamati ya uongozi Julias Mtatiro amesema; "... baadhi ya watu wanaomsaidia BWANA YULE kuivuruga CUF kuona kuwa bodi ya wadhamini imezuia njama za ufunguaji wa akaunti mpya ya CUF, wakatumia mbinu ya namna ile ile kwa njia tofauti."
Vilevile Mtatiro ameongeza kwamba, ili kufungua akaunti isiyo na uhusiano na kamati zilizoidhinishwa, za fedha ulisukwa mpango wa kuwaondoa baadhi ya viongozi wa cuf wilaya ya temeke kwenye utiaji saini unahousu akaunti mpya ili kwenda sambamba na na kuwageuza baadhi ya wateule wa Lipumba wanaofanya kazi za kukiujumu chama kutokea buguruni.
Fedha hizo kiasi cha shilingi 369,378,502.64 zimeibiwa ikiwa ni fedha za ruzuku kutoka kwenye akaunti ya chama, ambapo mmoja wa watu anayetajwa na Julias Mtatiro kuwa anahusika ni Mhina Masoud Omary ambaye ni mtu binafsi.
Hizi hapa chini ni barua ambazo msajili wa vyama vya siasa alimuandikia 'Mwenyekiti' na katibu mkuu wa cuf kuwajulisha kusitisha kukipatia chama hicho ruzuku kutokana na chama kutokuwa shwari;

Kufuatia sintofahamu hiyo chama cha wananchi CUF kupitia bodi ya udhamini kinalaani tukio hilo la utoloshwaji wa fedha hizo na kuelezea kusikitishwa zaidi na taasisi nyeti za kifedha kushindwa kusimamia utaratibu wao wa kiutendaji.
Post a Comment