Afya ya
jamii imekuwa ikipiganiwa kwa kiasi kikubwa kwa nchi na mataifa kutokana na
kuwa na umuhimu wa pekee kwa wananchi wa sekta zote, kwa mfano kujadili swala
la hedhi hadharani limekuwa ni kinyume na utamaduni wa watu wa taifa lolote
hasa la kiafrika.
ZAMBIA.
Nchini
Zambia hii
inaweza kuonekana ni kwenda kinyume na maadili ndio maana kuna sheria za
wafanyakazi zinazowaruhusu wanawake walio katika hedhi kuchukua siku moja ya
mapumziko inayojulikana 'Mother’s day' licha ya kwamba inasimamia wanawake wote
iwapo wana watoto au la.
Sheria hiyo haina masharti, wanawake wanaweza kuchukua siku
hiyo kwa matakwa yao wenyewe na sio lazima watoe kithibitisho chochote cha
kimatibabu, hatua inayowalazimu wengine kuhoji kuhusu sheria hiyo.
Ndekela Mazimba ambaye anafanya kazi katika idara ya
mahusiano ya umma anasema, ''Nadhani ni sheria nzuri kwa sababu wanawake hupitia
mengi wakati wanapokuwa katika hedhi''. Bi Mazimba hajaolewa wala
hana watoto lakini huchukua siku yake ya Mother’s Day kila mwezi kutokana na
uchungu anaopata wakati anapoingia katika hedhi.
''Unaweza kubaini
kwamba katika siku yako ya kwanza ya hedhi, unaweza kusikia maumivu mengi
katika tumbo, unaweza kununua dawa zote za kutuliza maumivu lakini unasalia
kitandani siku nzima, na mara nyengine, unagundua kwamba watu wengine wanahisi
uchungu siku za kwanza za hedhi, lakini siku zinaposonga uchungu unapungua.Mimi
hutaka kusaidiwa kwa siku za kwanza wakati ninahisi uchungu mwingi'',alisema Mazimba
Wanawake nchini Zambia hawalazimiki kufanya maandalizi
yoyote kabla ya kupumzika siku hiyo, lakini wanaweza kupiga simu siku hiyo
kusema wanachukua Mother’s day, lakini muajiri anayemnyima mfanyakazi wake siku
hiyo anaweza kushtakiwa.
Justin Mukosa ambaye amemuajili bi. Mazimba anaunga mkono
sheria hiyo na kusema kuwa anaelewa matatizo ya wanawake wanayokumbana nayo
wanapopima kati ya majukumu ya kifamilia na kazi, anasema hatua hiyo inaweza
kuwa na athari nzuri kwa kazi za wanawake.
''Utendaji sio tu mtu
aliye afisini. Unafaa kupimwa kulingana na uzalishaji wa mtu huyo''.
Lakini anakiri kwamba kuna matatizo katika mfumo huo
kutokana na kuwakosa wafanyakazi kupitia notisi fupi mbali na majaribio ya watu
kuuchezea. Unaweza kutumiwa vibaya kwamba pengine mtu ana jambo lake ambalo
anataka kufanya kwa hivyo anachukua Mother’s day.
Sio kila mtu anaunga mkono siku hiyo ya Mother’s Day na kuna
wanawake wengi miongoni mwao wanakosoa, Mutinta Musokotwane-Chikopela ameolewa
na ana watoto watatu, anafanya kazi ya ukuzaji lakini hachukui siku ya mother’s
day akisema kuwa inasababisha uvivu miongoni mwa wafanyikazi wanawake.''Siiamini na
siichukui, hedhi ni jambo la kawaida katika mwili wa mwanamke, ni sawa na kuwa
na mimba ama hata kujifungua'',alisema.
Nadhani wanawake huchukua fursa ya siku hiyo hususani kwamba
hakuna njia ya kuthibitisha kwamba uko katika hedhi au la.
Bi Chikopela anasema kuwa sheria hiyo inafaa kufanywa kuwa
wazi zaidi, ''Tatizo la Zambia ni kwamba kuna likizo nyingi sana, ikiwemo
likizo ya siku ya maombi, kwa hivyo nadhani Mother’s day inawafanya wale
wanaopenda likizo kufurahi''.
Source: BBC
Post a Comment