0
Waziri wa Maji na Mazingira Emmanuel Niyonkuru aliuawa usiku wa kuamkia Jumapili ya mwaka mpya Januari 1. 2017 alipokua akiingia kwenye gari nyumbani kwake kata ya Rohero katikati ya mji wa Bujumbura.
Manispa ya jiji la Bujumbura imebaini kuwa mauaji ya Waziri Emmanuel Niyonkuru yalifanywa majira ya saa saba usiku wa mwaka mpya, ambapo inasemekana mauaji hayo yalifanywa kwa kutumia siraha aina ya bastola.
Marehemu Emmanuel Niyonkuru enzi wa uhai wake.
Profile photo: Polisi wakiwa katika doria kwenye moja ya mitaa mjini Bujumbura.

BURUNDI.
Mapema jumapili asubuhi baada ya tukio hilo, Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: “Waziri Emmanuel Niyonkuru ameuawa usiku wa kuamkia leo. Rambi rambi zangu kwa familia yake na wananchi wa Burundi. Wahusika watahukumiwa kwa mujibu wa sheria.”
Vilevile mshauri mkuu wa Rais Pierre Nkurunziza Willy Nyamitwe aliponea chupuchupu kuuawa baada ya mlinzi wake kuuawa kwa risasi alipokua akirejea nyumbani kwake kilomita 6 kutoka mji wa Bujumbura mwezi mmoja uliopita.
Msemaji wajeshi la polisi nchini humo Pierre Nkurikiye ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa polisi inamshikilia mwanamke aliyekua akiambatana na Waziri Niyonkuru kwa ajili ya uchunguzi.
Pia imeendelea kusema imewakamata watu watatu ikiwa ni pamoja na mwanamke mmoja ambao inawatuhumu kuhusika na mauaji ya Waziri huyo, huku ikiongeza kuwa aliyetekeleza mauaji hayo hajulikani aliko.
Taarifa zinasema mauaji nchini humo yamekithiri huku watu wamekuwa wakipotea na baadaye kuokotwa kwa miili ya maiti zao na wengine kupelekwa sehemu kusikojulikana

Post a Comment

 
Top