 |
Neno/ishara
maarufu picha ya juu kabla ya kubadilishwa na kuwa hollyweed picha ya chini.
|
MAREKANI.
Kama
ni mfuatiliaji wa movie/sinema nyingi zinazotengenezwa nchini Marekani chini ya
eneo maarufu sana kama kiwanda kwa ajili ya kutayarisha mpaka kuzalisha
hutakosa kuelewa nazungumzia sehemu inayoiwa Hollywood ambayo ishara hiyo herufi zake zina
urefu wa futi 45 na inapatikana katika mlima Lee.
Los Angeles ndiko eneo
ilipo Hollywood na raia waishio eneo hilo ambao ndiyo majirani wa eneo la kuigiza filamu waliamka asubuhi
ya mwaka mpya na kuona ubao uliobeba ishara
‘Hollywood’ ya eneo hilo maarufu umebadilishwa na kuwa 'Hollyweed'. Herufi za ishara hiyo kwa
kuwa herufi 'O' zilifanywa na kuwa 'E.'
Wapiga kura
mjini California waliidhinisha sheria ya kuhalalisha bangi katika kura iliofanyika
wakati mmoja na uchaguzi mkuu wa nchini Marekani mnamo tarehe novemba 8.2016,
vyombo vya habari kutoka eneo hilo vimelipoti kuwa maofisa wa polisi
wanachukulia kitendo hicho kama jambo dogo na ni mzaha ambao haujaharibu kitu
pamoja na kwamba bado wanafanya uchunguzi.
Gazeti la
Los Angeles Times limeripoti kwamba mtu mmoja alirekodiwa akipanda katika
ishara hiyo ili kubadilisha herufi hizo, wafuatiliaji wa mambo wanasema tukio
kama hilo liliwahi kufanyika miaka ya 1976 ili kulegeza sheria dhidi ya bangi.
Post a Comment