0
“tunataka kuboresha mapato ya halmashauri zetu, sehemu zozote zenye hitilafu kutokana na makossa ya kukopi na kupesti basi inabidi sehemu zenye makossa zifanyiwe masahihisho tukiwa humu humu ndani”

Mwenyekiti wa balaza la madiwani la wilaya ya Meru Willy Njau mwenye kipaza sauti akiweka sawa kuhusiana na mjadara unaofanyika katika balaza hilo wilayani Meru.

Picha mbili juu >> Madiwani wakisikiliza michango na mijadara ya madiwani wenzao (hawapo pichani) kuhusu mapato na matumizi ya bajeti ya wilaya ya Meru.

Makamu mwenyekiti wa balaza la madiwani ndg Mafie akitanabaisha kuhusu posho za madiwani ambazo usafiri 50000, kujikimu 50000  kikao 70000 na kutokana na kwamba wao ndiyo wanaofanya maamuzi kuliko hata mtaalam.
Aman Sanga Afisa mifugo na Uvuvi wa wilaya akijibu swali kuhusu kupungua kwa mapato katika sekta ya mifugo na uvuvi willayani humo.
Picha juu >> Madiwani wakisikiliza michango wa Afisa mifugo na uvuvi (picha ya juu) kuhusu mapato yatokanayo na ofisi yake kwa wilaya ya meru.
Mganga mkuu wa wilaya ya Meru Ukio Kusirye akijibu swali lililohusu mapato yatokanayo na sekta ya afya wakati wa balaza hilo.
icha juu >> Madiwani wakisikiliza majibu yam ganga mkuu wa wilaya kuhusu mapato yatokanyo na sekta ya Afya (picha ya juu) kuhusu mapato yatokanayo na ofisi yake kwa wilaya ya meru.
Mwakilishi wa Katibu mkuu tawala mkoa wa Arusha Moses Mabula akiondoa wasiwasi kwa madiwani kuhusu kuwepo kwa mapungufu mengi katika bajeti


MERU.

Baraza la madiwani wa wilaya ya Meru linakaa kujadili bajeti yam waka 2017/18 huku kukiwa na changamoto mbalimbali zilizopo wilayani humo zikiwemo kupungua kwa mapato katika baadhi ya biashara kama nyumba za wageni, kwenye masoko yaliyopo wilayani hapo pamoja na baadhi ya biashara kufungwa hivyo, kuwepo kwa baraza hilo ni kuweza kuinua mapato ya Halmashauri hiyo.

Vile vile ili kuweza kukuza mapato ya wilaya hiyo ambayo ina zahanati binafsi kadhaa ambazo nazo zinachangia pato la wilaya hiyo, hivyo Mganga mkuu wa wilaya Ukio Kusirye ambaye anajibu swali lililoulizwa kuhusu tozo na ada zinazotozwa kwa zahanati ndogondogo zilizopo katika wilaya ya Arumeru ikiwa ni pamoja na upimaji wa Afya kwa watoa huduma wa zahanati hizo.

Afisa mifugo na uvuvi wa wilaya ametanabaisha kutokuwepo kwa mapato ya uhakika kutokana na bidhaa za uvuvi kama samaki, ikiwa na maana katika wilaya hiyo hakuna uvuvi unaofanyika labda kwa kutegemea bidhaa zinazopita katika wilaya hiyo.

Kumekuwepo na makusanyo hafifu yanayopatikana katika soko la kisorongo lililopo wilayani humo, ambapo meneja biashara wa soko hilo ameshindwa kujibu nyumba za wageni pamoja na kuwepo na mapato mengi kwa kipindi kilichopita lakini muda sasa mapato yamepungua pamoja na kwamba diwaniKwa niaba ya kinaendelea kufanyika katika ofisi za wilaya ya meru mkoani Arusha.

Idara ya biashara inacheza katika siasa chafu ikipelekea hata kumfedhehesha Rais Magufuri kutokana na tabia hii, hali hii inatokana na kufuatilia mara kadhaa, “taarifa hii ya mapato ya ndani yapaswa tuikatae ili ikarekebishwe maana haina muelekeo wenye kuleta tija kwa maendeleo ya wilaya yetu” anasema Romani diwani wa kata ya keri.

Wakati asilimia 94 ya bajeti ya halmashauri ya wilaya ya Meru bado ni tegemezi kutoka kwa serikali kuu mwakilishi wa katibu tawala wa mkoa wa Arusha “tunataka kuboresha mapato ya halmashauri zetu, sehemu zozote zenye hitilafu kutokana na makossa ya kukopi na kupesti basi inabidi sehemu 

Post a Comment

 
Top