0
Moja ya kauli ya Rais wa sasa wa Marekani Donald Trump ni kuwaondoa waislam hama kuwasajili wote waliopo nchini humo ili kuweza kuwafuatilia, kutokana na kauli hiyo inayoonekana kuwa ya kibaguzi imepelekea watu mbalimbali duniani kutoa kauli mbalimbali.

Madeleine Albright, ambaye amejitoa kujisajaili kuwa muislame endapo... 


MAREKANI
Aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani na mwanasiasa machachari Madeleine Albright na msanii Mayim Bialik wa Bing bang wameapa kujisajili kuwa Waislamu iwapo Donald Trump ataanzisha usajili wa waislamu pekee.
''Nilililewa kama mkatoliki nikawa Episcopalian na baadaye nikabaini kwamba familia yangu ilikuwa ya Kiyahudi'', Bi Albright, ambaye ni mwanamke wa kwanza kuwa waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani alisema katika mtandao wake wa Twitter.
Tamko lake hilo limekuja huku kukiwa na uvumi kuhusu agizo la rais ambalo litafanya kuwepo kwa ukaguzi wa kina, kupiga marufuku wakimbizi mbali na watu wanaoingia kutoka nchini humo kutoka mataifa saba ambayo yatashirikisha Syria,Yemen na Iraq.
Lakini bado hakujawa na usajili wa wamarekani waislamu katika miezi ya hivi karibuni, swala ambalo bwana Trump alisema atalitekeleza katika mahojiano aliyoyafanya mwaka 2015 kabla ya kukana kufanya hivyo hivi karibuni.



Source BBC

Post a Comment

 
Top