ARUSHA.
Na Michael Nanyaro.
Katika tukio la kuuwawa
kwa wafugaji walioingiza mifugo yao katika eneo la msitu unaolindwa na askari
wa JKT, wafugaji kadhaa waliuwawa kutokana na mashambulizi yaliyotokea kutoka
na kukamatwa kwa mifugo yao.
PICHA JUU >> Baadhi ya wananchi wa
kata ya oldonyosambu wilaya ya Arumeru mkoani Arusha wakiwa wamekusanyika
katika eneo la ofisi za kata hiyo kufuatia kuuwawa kwa mwenzao na askari wa
jeshi la kujenga taifa (JKT) waolinda msitu jirani wa mlima meru, jumla ya
wafugaji watano walipoteza maisha na wengine saba kujeruhiwa usiku wa kumakia
juzi.
| Viongozi wa serikali wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Alexander Pastor Mnyeti mwenye shati la Bluu wakiwa eneo la tukio kwa ajili ya kuongea na wananchi kuhusiana na tukio. |
Katika hatua nyingine
inayoonyesha majonzi kwa wafugaji hao, mmoja wa marehemu ambaye aliuwawa majuzi
mazishi yake yanatarajiwa kufanyika leo ambapo wananchi wa eneo la kata ya
oldonyosambu wanakusanyika kwa ajili ya kumuaga mwenzao.
Post a Comment