0
Utendaji kazi wa mfumo wa mwili wako kutokana
na vile unavyoulisha na kufanyisha mazoezi.


Kushambuliwa kwa kuta za pembeni mwa moyo na ambazo zinaweza kuzuia damu kupita kwenye mishipa na selli tishu kupata chembe chembe nyeupe (white blood cell) Atherosclerosis pia ni sababu inayooneka kuwa ya kawaida ya ugonjwa wa moyo na mishipa. Yote hayo husababishwa na matatizo correctable, kama vile chakula kibaya, kutokufanya mazoezi, uvutaji wa sigara hata uzito usio wa kawaida.


Moyo ndiyo kiungo chenye nafasi ya kipekee katika kufanya kazi ya kusukuma damu na kazi nyingine mwilini.

AFYA YA JAMII.
Kulingana na ripoti ya shirika la Afya Duniani (WHO), inaonyesha robo ya watu wazima waliopo nusu ya nchi za Afrika ambazo zimefanyiwa utafiti wana angalau sababu tatu zinazoonyesha hatari zinazoongeza uwezekano wa kuwa na moja au zaidi ya magonjwa ya moyo wakati wa maisha yao.
Shinikizo la damu ni ugonjwa ambao umeota mizizi barani Afrika na asilimia zaidi ya 10 ya wananchi wa afrika wanakabiliwa na ugonjwa wa moyo. Wakati ambapo matumizi ya tumbaku au sigara na pombe yapo katika kiwango cha chini barani Afrika kuliko sehemu zingine duniani, shinikizo la damu lipo katika kiwango cha juu zaidi duniani, na kuathiri karibu nusu ya ya watu wazima.
Kuna njia kadhaa ambazo wataalam wanasema ukitumia unaweza kuepukana na madhara ya kupatwa na ugonjwa huu endapo utafanya; Mazoezi ya aina tofauti, kula matunda angalau matano na mboga za kijani kwa siku, kutotumia tumbaku au sigara na pombe, hizo ni moja ya njia za kupambana na ugonjwa wa moyo, kansa au kisukari.
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa wanawake wa Afrika wenye umri wa zaidi ya miaka 45 wako katika hatari zaidi ya kuambukizwa magonjwa hayo, vilevile kiwango hicho kinatisha kwa sababu ugonjwa huo unaathiri pole pole na mara nyingi unagunduliwa baada ya miaka kadhaa.
Hata hivyo matatizo yote haya ya afya yanaweza kuzuiwa kwa kula vizuri na kufanya mazoezi, kama tahadhari hizi hazizingatiwi, hali hii inaweza kupelekea serikali kutumia mabilioni ya pesa katika kugharimia matibabu ya magonjwa hayo.



Post a Comment

 
Top