Picha ya X-ray ikionesha kisu kilivyo tumboni
mwa mbwa huyo.
|
Mbwa huyo wa umri wa wiki 12 kwa jina Macie,
alikimbizwa kwa daktari wa mifugo kwa huduma ya dharura baada ya kuanza
kukohoa, Mbwa ambaye alimeza kisu cha
urefu wa sentimita 20 anapata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji.
Mwenye mbwa huyo anasema alidhani kuwa alikuwa amemeza
kifaa cha kuchezea cha watoto, lakini X ray baadaye ilionyesha picha ya kisu
kikuwa tumboni.
Daktari ambaye amekuwa
akimtunza mbwa huyo tangu afanyiwe upasuaji anasema ana habati sana kuwa hai,
hata hivyo mmiliki wa mbwa huyo kutoka Glasgow alikuwa amempoteza mbwa wake
mwingine kutokana na ugonjwa wa saratani/kansa.
Siku moja baada ya kufanyiwa upusuaji alionekana
mchangamfu. Mbwa huyo amekuwa akirudishwa kwa daktari kufanyiwa ukaguzi kwa
muda wa wiki mbili na sasa anaendelea kupata nafuu.
Mara baada ya kufanyiwa
upasuaji na kutolea kisu hicho kutoka tumboni.
|
Sourse BBC.
Post a Comment