0
Baraza kuu la waislam nchini BAKWATA limewataka waislamu wote nchini kurejea kwa mwenyezi mungu na kumlilia ili kulinusulu taifa kutokana na hali ya ukame ambayo inaoneka kulikumba na kusababisha njaa kwa maeneo kadhaa hapa nchini.


Sheikh Khamis Mataka –Msemaji wa Bakwata nchini akiongea na wanahabari (hawapo katika picha) juu ya mustakabali wa taifa kutokana na baa la njaa linaloonekana kuinyemelea nchi.
Baadhi ya viongozi wa Bakwata kutoka kulia ni Sheikh Khamis Mataka, Sheikh Suleimani Lolila ambaye kwa sasa anastaafu kutokana na umri, Sheikh Abubakar Alfan –Mshauri wa Sheikh mkuu wa Tanzania na mwisho kushoto ni Sheikh Hassan Chizenga.


DAR ES SALAAM
Katika taarifa yake Mufti mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar bin Zubeir, iliyosomwa na Sheikh Khamis Mataka ambaye ameteuliwa (kwa sasa) kuwa msemaji wa Mufti mkuu na waislam kwa ujumla, amewaomba waislam wote kwa ujumla kuleta toba, kumuomba msamaha Mwenyezi Mungu na kumuomba aijalie nchi yetu pamoja na nchi majirani kupata mvua za kheri zitakazosaidia kuepukana na ukame na madahra yake likiwemo baa la njaa.

 Pamoja na hilo Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar bin Zubeir ameongeza nafasi za kiutendaji na kufanya uteuzi wakwa nafasi kadhaa ikiwemo nafasi ya msemaji wa rasmi wa Balaza kuu la Waislamu wa Tanzania –Bakwata, ambapo Khamis Said Mataka na Sheikh Hassan Said Chizenga wanachukua nafasi hizo ambapo hapo awali ilikuwa haina mtu.

Sheikh Hassan Chizenga kwa sasa ni Mkurugenzi wa Daa’wa na Tabligh Bakwata na Sheikh Abubakar bin Zubeir ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Halmashauri kuu ya Bakwata.

Vilevile      Sheikh Mataka amesema; kumekuwepo na matumizi yasiyo sahihi ya wadhifa wa ‘Sheikh Mkuu’ ambapo imekuwa ikitumika na baadhi ya masheikh wa mikoa na wilaya pasipo kuelewa, ambapo kwa mujibu wa balaza kuu la Waislam nchini –Bakwata wadhifa wa Sheikh mkuu unamuhusu Mufti wa Tanzania tu na si mwingine yeyote, hivyo basi amewasihi masheikh wa mikoa, wilaya, na mitaa kutambua hilo na kuwakumbusha kutumia nyadhifa zao kama zilivyoainishwa katika katiba ya Balaza Kuu la Waislam Nchini. (Bakwata)



Post a Comment

 
Top