0
Wanamgambo wa kundi la al-Shabab wamewaua kwa kuwapiga risasi watu watatu, wawili kati yao kwa makosa ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja kusini mwa Somalia na mwanamume wa tatu aliuawa kwa kufanya ujasusi dhidi ya kundi hilo.



SOMALIA
Sheikh Mohamed Abu Abdalla ambaye ni gavana mwanachama wa al-Shabab alisema Isak Abshirow -20 na Abdirizak Sheikh Ali -15 walifumaniwa na wapiganaji wa al-Shabab wakifanya mapenzi, watu hao wanaaminika kuwa watu wa kwanza kuuawa na al-Shabab kwa makosa ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja.
Saeed Mohamed Ali alipatikana na kosa la kuvifanyia ujasusi vikosi vya Ethiopia ambao ni sehemu ya kikosi cha wanajeshi wa Muungano wa Afrika wanaokabiliana na wanamgambo hao. Watu hao waliuawa hadharani na katika mji Buale ambako umati mkubwa wa watu ulikuwa umekusanyika.
Mtandao mmoja uliofungamana na kundi hilo, umeripoti kuwa mahakama ya Kiislamu katika eneo la Jubba iliwakuta na hatia watu hao. Kushiriki mapenzi ya jinsia ni hatia kisheria katika mataifa mengi ya Afrika na hukumu yake huwa ni kifungo grezani.
 "Jaji alitoa hukumu kwa wanaume hao watatu hadharani na kuwakuta na hatia. Walipigwa risasi na kuawa katika mji wa Buale," Sheikh Abdalla, aliliambia shirika la habari la Reuters.
Afisa mmoja wa serikali ya Somalia amesema kuwa kesi yoyote inayohusu mapenzi ya jinsia moja nchini Somalia hushughulikiwa kwa mujibu wa Sharia katika taifa lenye idadi kubwa ya waumini wa dini ya Kiislamu, pamoja na hayo hakufafanua jinsi sheria hiyo itakavyotekelezwa.


Source rfi

Post a Comment

 
Top