Soko la hisa la Dar es
Salaam –DSE
limesema kuwa ongezeko la hati fungani katika soko hilo limetokana na baadhi ya
wawekezaji kutafuta hathari ndogo zaidi za bei ya hisa.
Meneja masoko, biashara na Mauzo wa DSE
akifafanua jambo alipokuwa akiongea na wanahabari mapema leo jijini Dar Es
Salaam.
|
DAR ES SALAAM.
Akizungumza na
wanahabari jijini na Dar Es Salaam meneja biashara na mauzo Patrick Msusa
amesema kuwa hatua hiyo ya ongezeko la hati fungani limesababisha mauzo ya hisa
katika soko hilo kushuka kutoka shs 13.2 bilion mpaka kufikia shs 8bilioni.
“hatua hii pia imeweza kusababisha makampuni matatu katika sekta
ya mawasiliano kuingia katika orodha ya makampuni ya simu yaliorodhoshwa katika
soko letu la hisa, ikiwemo Vodacom, Tigo na Airtel”. Alisema
Patrick Msusa.
Vile vile ameongeza kwa
kusema kuwa, katika takwimu za soko hilo kwa kipindi caha wiki sita zilizopita
ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani umeweza kupungua kwa asilimia 2.4% wakati kampuni ya TBL
ikiongoza kwa punguzo la asilimia 5% na sekta za kibiashara ikishuka kwa
asilimia 15.6% ambapo hatua hiyo imetokana na kushuka kwa hisa za benk ya CRDB.
Hata hivyo aliyataka makampuni
ya mawasiliano ya simu nchini kuweza kujiorodhesha kufuatia sheria ya serikali
ya kuyataka makampuni hayo kuuza hisa za zao kwa wananchi kupitia soko hilo ili
kukuza na kuchangia katika pato la taifa.
“hadi sasa tunayo orodha ya makampuni ya mawasiliano ya simu za
mkononi matatu tu hivyo basi napenda kutoa wito kwa makampuni mengine kuweza
kujiorodhesha katika soko letu” aliongeza
Msusa.
Msusa aliongeza kuwa
suala la kushuka kwa mauzo ya hisa
katika soko hilo limetokana na mdororo wa kiuchumi kwa siku za hivi karibu
kuliyo yakumba baadhi ya makampuni hapa nchini.
Post a Comment