0
 ••Madaktari wanaonya ulaji wa pipi kazini kuwa ni tishio kwa Afya.
Watu wengi wamekuwa wakienda na wakati kwa kutaka kuonekana kwa wengine kuwa wapo tofauti nao kwa kwenda kisasa si kupitia mavazi hama kitu kingine cha ajabu ila ni kupitia viburudisho vyenye wingi wa sukari, madaktari wa meno wameshtumu utamaduni wa watu wawapo kazini wakisema ugawanyaji wa keki na peremende/pipi unachangia matatizo ya kiafya.

••Aina kadhaa ya peremende/pipi.
Idara ya afya ya meno imesema kuwa watu wanatakiwa kupunguza ulaji wa keki, peremende, biskuti kazini kwa sababu vyakula hivyo vinawafanya kunenepa kupitia kiasi mbali na afya mbaya ya mdomo. Wafanyakazi wanahitaji kubadilisha utamaduni wawapo kazini.

Ili kuweza kupunguza ulaji wa vyakula vyenye sukari wafanyakazi wanashauliwa kutumia vyakula hivyo kama chakula cha mchana badala ya kuvificha .

Muhadhiri wa chuo kikuu cha Royal College of surgeons profesa Hut yeye anasema kuwa huenda wasimamizi wa ofisi au mameneja wanaotaka kuwazawadi wafanyikazi au wafanyikazi wanaotaka kusherehekea 'sherehe' hama mtu anayeleta zawadi ofisini baada ya likizo hatua hiyo nayo inasababisha vyakula vyenye sukari nyingi kuingia afisini.

Madaktari wanasema ulaji wa vyakula vya sukari unapaswa kusitishwa, kwani hilo linaathiri afya ya wafanyakazi na ni muhimu kufanya uamuzi kwa mwaka mpya kukabiliana na utamaduni wa vyakula vyenye sukari.

''Ijapokuwa peremende hizo huenda zikawa na maana, lakini zinachangia unenepaji wa kupitia kiasi pamoja na afya mbaya ya mdomo ikiwa ni kuoza kwa meno na kutoboka na baadaye kubaki kibogoyo'' aliongezea prof. Hut
Tunahitaji kubadili utamaduni katika ofisi zetu ambao utashawishi ulaji wa vyakula vinavyoupa mwili afya na unamsaidia mfanyakazi kutotumia vyakula vyenye sukari kama vile keki, peremende na biskuti.

Post a Comment

 
Top