0
Gavana Kivutha Kibwana wa Makueni.
NAIROBI.
Kwa muda sasa wabunge na maseneta wamesikika wakitoa matamshi ya kukejeli maagizo ya mahakama na ushauri wa mwanasheria mkuu wa serikali, visa vya hivi karibuni ni tukio la kuwahoji mawaziri mbele ya kikao cha bunge, vilevile maagizo ya mahakama kuhusu kutimuliwa kwa Gavana Kivutha Kibwana wa Makueni nchini Kenya.
Maseneta hao wamekuwa wakilalamikia kutishiwa na polisi waliokuwa wamelizingira jengo ya bunge la seneti la nchi hiyo, lakini wajuzi wa sheria wanasema mienendo hiyo inafaa kukoma kwa kuwa ni mfano usiofaa kwa wakenya, aidha, polisi waliweka vizuizi mbalimbali katika barabara ya kuingia bungeni.

Profile photo: Ukumbi wa bunge la kenya.
Maseneta hao walikuwa wamekusanyika kwa ajili ya kikao maalum cha kujadili sheria ya uchaguzi, wameeleza kughadhibishwa na hatua ya polisi kuwadhalilisha bungeni, vile vile wamejitetea kuwa polisi waliojihami walimiminika sehemu mbalimbali ya bunge hilo, jambo si la kawaida.
"Tunalaani vikali hatua ya polisi kuzingira bunge la Seneti na yeyote aliyehusika kuwapa mamlaka ya kuzingira bunge siku hii, anastahili kuchukuliwa hatua". Alisema kiongozi wa waliowengi katika Seneti, Kithure Kindiki.
Seneta kutoka mrengo wa serikali, Kipchumba Murkomen, alisifu hatua ya kuwepo kwa polisi hao na akasema. "Tujilaumu wenyewe kwa mienendo yetu, tunaingia bunge tukibeba visu, pilipili na hata filimbi wabunge wenzetu wanamtusi Rais ni aibu".

Siku kadhaa zilizopita, bunge la taifa hilo lilishuhudia vurugu baada ya wabunge wa upinzani kujaribu kumzuia spika Justin Muturi kuingia bungeni wakipinga mjadala wa kubadilisha sheria za uchaguzi. Hata hivyo seneta Hassan Omari alipendekeza kikao hicho kivunjwe hadi polisi watoke bungeni.



Post a Comment

 
Top