DAR
ES SALAAM.
Usafiri ni sehemu mojawapo ya kujongea kutoka sehemu
moja na kuelekea sehemu nyingine huku chombo chochote kinachoweza kukusafirisha
sehemu husika kwa lengo linalofanya kwenda hapo, hii ni sehemu ya maisha ya
binadamu inayofanya neno usafiri kuwepo kwenye mfumo mzima wa maisha ya kila
siku.
![]() |
Safari za mwanzo kabisa kusafiri hapa Africa.
|
Hii inatokana na binadamu kukaa na kutafakari nini kifanyike kupunguza urasimu wa kupoteza muda wa kutembea, hata hivyo pamoja na kuwepo kwa mazingira ya kupunguza muda wa mtu kutoka eneo moja mpaka lingine, teknolojia ilileta chombo kijulikanacho kama pikipiki ya magurudumu mawili, hiki ni chombo kilichokuja kusaidia kupunguza muda na kuharakisha safari, kwa nchi za kiafrika imekuwa ni msaada mkubwa ikiwa na maana hata kule chombo kingine kisipoweza kufika kutokana na njia, ufinyu wa eneo pamoja na gharama, basi chombo hiki kinaweza kufika kwa wakati na kwa garama ya chini.
![]() |
Profire phtoto: Hii ni baada ya harusi, safari inaanza.
|
Hata
hivyo uwepo wa chombo hiki hususani hapa nchini umekuwa na faida na hasara zake
kutokana na matumizi yanayotumika tofauti na watengenezaji wake hama sheria za
nchi kinapotumika.
Hapa nchini kumekuwa na
baadhi ya waendesha pikipiki hizo maarufu (Bodaboda) wakitumia chombo hicho tofauti
na uwiano mahususi, kutokana na hilo waendeshaji wengi hama abilia waliowahi
kubebwa wamebaki hawana moja ya kiungo cha mwili kutokana na ajali iliyotokea
kutokana na kutofuata utaratibu unaopaswa, hivyo kupelekea makosa na maumivu
kwa mhusika.
Hapa
chini TODAYS NEWS tumekuwekea picha kadhaa zikionyesha moja matumizi yasiyo sahihi kwa pikipiki ya magurudumu
mawili iliyoweza kubeba abilia na muendeshaji wake kufikia watu sita (6), hapo
ni eneo la Mbagara Kisewe, ambapo ilipouliza kwa vijana wengine ambao
walishuhudia hali hiyo tulipata hili hapa, “kaka hali hii sisi wenyewe hatuipendi ila inatokana na
abilia mwenyewe anakuja na wenzanke kama unavyoona anakwambia tunaenda sehemu
fulani tuna shs 1000/- ukiangalia bosi anasubili hesabu na sehemu wanapokwenda
siyo mbali basi unawapelekea hivyo hivyo tu”
alisema Mohamed mmoja wa waendeshaji wa bodaboda wa eneo hilo.
Hii ni pikipiki inayoruhusiwa kubeba watu wawili lakini hapa
imeweza kubeba watu sita kwa mara moja kitu ambacho si kawaida.
|
Mpita njia akipita karibu na pikipiki iliyobeba watu sita, kupitia picha hii ndipo unaweza kuwaona wote waliobebwa, mbele ni (1) kijana mdogo, anayefuatia ni (2) dereva wa pikipiki hiyo, nyuma yake kuna (3) binti mdogo kavaa ushungi wa bluu,anayefuatia (4) mwenye kilemba cha njano kuna (5) mtoto wa kike anaonekana kichwa ambapo wa mwisho ni (6) dada mwenye ushungi mwekundu na ameshika kikapu.
|


Post a Comment