Akishikiliwa na maofisa usalma wa marekani.
|
MAREKANI:
Kumekuwepo na matukio kwa baadhi ya raia wan chi mbalimbali kutaka
kufanya uharifu wa kuwadhuru viongozi wakuu wa nchi ikiwa ni kuwatamkia maneno yenye
kutia hofu hama kwa kutaka kutumia siraha.
Nchini marekani kijana mmoja raia wa Uingereza amehukumiwa kifungo cha
miezi 12 jela kufuatia jaribio lake la kutaka kunyakua bunduki kwa lengo la
kumuua Rais mtarajiwa wa Marekani Donald Trump.
Michael Sandfgord mwenye umri wa
miaka 20 alikiri kosa hilo la kumiliki bunduki na kuvuruga mkutano, pia analaumiwa
kwa kujaribu kunyakua bunduki kutoka kwa polisi, ambapo jaribio hilo la kunyakua
kutoka kwa afisa wa polisi
halikufanikiwa wakati wa mkutano wa hadhara huko Las Vegas ili kumfyatulia
risasi mgombea urais.
Mahakama ilisema kuwa huenda akaachiliwa baada
ya miezi minne ambapo atasafirishwa hadi nchini Uingereza, mara baada ya
Sandford kukamatwa aliwaambia maafisa kuwa alikuwa na mpango wa kumpiga risasi
Donald Trump.
Akiwa na familia yake
mama yake na mdogo wake
|
Mama mzazi anasema alipoteza
mawasiliano na mwanaye toka mwaka 2015 pale alipoondoka nyumbani akienda
kutembea huko marekani.
Kulingana na nyaraka za mahakama, kijana huyo
Sandfords ambaye hakuwa na makao na ambaye alikuwa akiishi nchini Marekani
kinyume cha sheria baada ya muda wa visa yake kuisha, aliiwaambia majasusi kuwa
aliendesha gari kutoka California hadi Nevada kwa lengo la kumpiga risasi
Trump.
Anaripotiwa kumuambi afisa wa polisi kuwa alitarajia
kuuawa kwenye shambulizi hilo na kwamba alikuwa na tiketi za kuhudhuria mkutano
mwingine wa Trump baadaye ikiwa angepata nafasi ya pili, majaji walisema
kitendo hicho ni cha kustaajabisha.
Post a Comment