0


Kaimu mkuu wa chuo cha mipango na maendeleo vijijini Prof. Israel Katega akimkaribisha Waziri wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Ufundi PROF. Joyce Ndaalichako mara baad aya kuwasili kufungua na kusikiliza maoni ya wakuu hao wa shule za sekondari nchini.
Rais wa chama cha walimu wakuu wa shule za sekondari nchini (TAHOSSA) Bonus Ndimbo aliyesimama akiongea na Waziri wa Elimu Prof. Ndarichako (kulia) katika ofisi za Mkuu wa chuo cha Mipango na Maendeleo vijijini kuhusu mkutano mkuu wa chama chao, wengine ni viongozi wa chama hicho.
Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako aliyenyoosha mkono akiwasalimia wanachuo wa chuo cha Mipango na Maendeleo vijijini (hawapo pichani) alipokuwa akielekea ukumbini, wengine ni viongozi waandamizi wa chama hicho akiwemo mkuu wa wilaya ya Dodoma Christina Mndeme kushoto.
Kulia ni Bonus Mndeme Rais wa chama cha walimu wakuu wa shule za sekondari nchini, katikati ni Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako na kushoto ni Daima Matemu wakiingia kwenye ukumbi wa mkutano mkuu wa mwaka.

Rais wa (TAHOSSA) Bonus Ndimbo akisoma risala kwa mgeni rasmi juu ya mkutnao huo ambapo alitoa pongezi kwa Rais Magufuri kwa kutimiza mwaka mmoja madarakani pamoja na kuiomba serikali kwa kutoa kibali kufanyika mkutano huo.

Baadhi wa wanachama wa TAHOSSA ambao ni wakuu wa shule za sekondari nchini wakimsikiliza Rais wa chama chao alipokuwa akiwasilisha risala kwa mgeni rasmi mjini Dodoma.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christina Mndeme akiwakaribisha wajumbe wa mkutano mkuu wa TAHOSSA, lakini aligusia mapambano dhidi ya mimba kwa wanafunzi walio mashuleni katika wilaya yake ambapo amegusia wilaya yake kuwa na wanafunzi wapatao 52 wenye hali hiyo.
Viongozi waandamizi wa chama cha walimu wakuu wa shule za sekondari nchini TAHOSSA wakifuatilia na kuandika yale yaliyokuwa yanawasilishwa na Rais wa chama chao.
Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako akiongesa katika mkutano huo ambapo aweka wazi msimamo wa serikali katika kutimiza wajibu wake kwa shule za serikali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila shule inapata vifaa vya mahabara mara vitakapofika nchini, kulia ni viongozi wa TAHOSSA.
Wakuu wa shule za sekaondari nchini ambao ni wanachama wa TAHOSSA wakimsikiliza waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani).
Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako (wan ne kushoto), mkuu wa wilaya ya Dodoma Christina Mndeme (wa tatu kushoto), Rais wa TAHOSSA Bonus (wa kwanza kushoto) anayemaliza muda wake wakiwa katika picha ya pamoja kwa ajili ya kumbukumbu na viongozi wa TAHOSSA na walimu wakuu wa kanda mbalimbali za mkutano mkuuwa chama uliofanyika mjini Dodoma Disemba 14-15 2016.




Post a Comment

 
Top