Rais
wa chama cha walimu wakuu wa shule za sekondari nchini Bonus Ndimbo akifungua
mkutano mkuu wa mwaka unaofanyika katika ukumbi wa chuo cha mipango na
maendeleo vijijini mjini Dodoma.
|
Mwenyekiti
wa TAHOSSA nchini ndg Bonus Ndimbo (kulia) akiteta jambo na Daima Matemu -katibu mkuu wa
chama hicho wakati wa michango na mjadara wa mapato na matumizi ya chama hicho.
|
HABARI KWA UNDANI:
DODOMA:
Mkutano mkuu wa chama
cha walimu wakuu wa shule sekondari nchini (TAHOSSA) umekutana mjini Dodoma
ukiwa na lengo la kujadili na kuweka mikakati inayoweza kuweka malengo ya chama
na kufanya uchaguzi wa uongozi katika chama hicho.
Pamoja
na kuwepo kwa mjadara mzito unaohusiana na mapato na matumizi ya chama hicho
kutoka kwa wanachama kwenda kwa viongozi wa chama hicho, baadhi ya changamoto
hizo zinaweka nafasi ya kuweka mipango endelevu ili chama kijikite katika
uwekezaji na maendeleo.
Naye katibu msaidizi wa
TAHOSSA nchini Martha Minde amezungumzia maendeleo yaliofikiwa kutokana na
maazimio yaliyofikiwa kutokana na wakuu wa shule kutekeleza ikiwemo na uhusino
mzuri kati ya wakuu wa shule na wadau wa elimu, viwanja vya michezo utakaoambatana
na uendeshaji wa michezo ya umisseta nchini.
Ameongeza kuwa maeneo mengi ambayo walimu wanapaswa
kusimamia ni katika suala la Mazingira (Tabia nchi) ambalo limekuw ni tatizo
kubwa la dunia ambapo kauli mbiu ya ‘MTI WANGU’ imepewa nafasi kwa kila mtu
aliye shule apande mti, kupitia hatua hiyo imekuja na kauli mbiu ya “mtu mmoja mti mmoja” hata
hivyo amesisitiza kuwepo kwa elimu ya
maambukizo ya ukimwa iendelee kutolewa kwa wanafunzi na watumishi wote shuleni.
Pia
mwenyekiti amewashukuru wajumbe kutokana na muda wake kuisha na kuwataka
ushirikiano kwa wakati wote atakapokuwa hayupo kiungozi kapitia umioja huo,
amesema mambo kadhaa kuhusiana na wale wanaorusha mawe kwa serikali akitolea
mfano wa msemo wa Mwalimu Nyerere ‘serikali ipo haijalala’ hivyo amewasihi
wanachama kutumia majadiliano na kuisikiliza serikali bada la ya kulaumu.
Wanachama wa TAHOSSA ambao ni walimu wakuu wa shule za sekondari nchini
wameweza kuchangia mambo mengi, lakini moja kati ya lililopewa nafasi ni
kuhusiana na mapato na matumizi, ikiwa ni pamoja na safari zisizo na maana ambazo
viongozi wanaweza kuzifanya, lakini nafasi ya kuwa na mfumo wenye nguvu, kuongeza
wanachama na michango itakayoweka nafasi ya kuwa maendeleo kupitia uwekezaji.
Lakini pia mmoja wa
wanachama katika kuchania amesema, changamoto zilizopo zikiondolewa serikali
inaweza kutia mkono hata kupitia uwekezaji wa jengo tunalolitaka, maana sehemu yeyote yenye migogoro serikali
hawezi kuweka mkono wake kusaidia maendeleo. Vile vile nafasi ya wanachama wanaotoka katika chama wapewe nafasi ya kupata hisa ili wawe wanachama kwa baadaye.
Post a Comment