Mwenyekiti
wa bodi ya wadahamani wa Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi Emmanuel Humba
akizungumzia uzinduzi na uwezeshaji wautoaji wa huduma kwa mfuko huo.
|
Mwanamuziki
wa nyimbo za asili nchini Mrisho Mpoto akitumbuiza katika uzinduzi wa huduma za
utoaji wa mafao ya faida kwa wafanyakazi katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa
wa kisenga.
|
Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa huduma za utoaji mafao ya fidia kwa waafanyakazi nchini Masha Mshumba akisisitiza jambo |
Wageni
waalikwa waliohudhulia uzinduzi huo wa moja kati ya mifuko tisa ya hifadhi ya
jamii nchini wa WCF Kisenga Hall makumbusho jijini Dar.
|
Naibu
waziri wa Antony Mavunde akifafanua jambo katika uzinduzi huo mapema jijini Dar
kuhusiana na faida kwa waajili kuwawekea wafanyakazi wao mafao.
|
Katibu
mkuu wa chama cha wafanyakazi Dr. Msigwa akiwasilisha salamu na uzoefu wa
matatizo wanayopata wafanyakazi yatokanayo na ajali kazini.
|
Mkurugenzi
mkuu wa chama cha waajili nchini (ATE) Dr. Mlimka akiongea katika uzindizu huo.
|
Mh.
Jenister Mhagama akitoa hotuba kwa niaba ya mgeni rasmi (waziri mkuu) alipokuwa
akizindua mfuko wa hifadhin ya jamii jijini Dar Es Salaam.
|
Akikata
utepe kwa niaba ya waziri mkuu Mh. Jenista Mhagama, kushoto kwake ni Mh. Antony
Mavunde.
|
Mara
baada ya kukata utepe kuashilia uzinduzi wa mfuko huo, kulia ni Mh. Jenista
Mhagama, Antony Mavunde nyuma, Abdallah Possi na nyuma ni Emmanuel Humba.
|
Wakisoma
maelezo yanayotolewa na mfuko huo wa huduma kwa wafanyakazi - WCF.
|
Mh.
Jenista Mhagama akitoa cheti cha utambulisho bora kwa watoa huduma bora wa
huduma za bima INSURANCE TANZANIA LIMITED AAR.
|
Mgeni
rasmi aliyekaa katikati kwenye meza kuu pamoja wa watoa huduma kwa jamii ambao
walipewa vyeti vya utambulisho.
|
HABARI KWA UNDANI:
DAR
ES SALAAM.
Serikali imesema inatambua mchango wa
sekta ya mifuko ya hifadhi ya jamii nchini katika kuhakikisha watumishi
wanakuwa na maisha bora mbeleni.
Kupitia sheria ya
mifuko ya hifadhi za jamii ya mwaka 2015 pamoja na tangazo la serikali namba
212A la tarehe ambayo imefanyiwa
marekebisho mwaka 2015 ambayo inahitaka mifuko ya hifadhi jamii nchini kuondoa
mapungufu yaliyokuwepokwenye sheria ya zamani ya fidia ambayo ilikuwa
ikilalamikiwa sana kutokana na kutoa malipo kidogo pamoja na ucheleweshwaji wa
mifuko hiyo.
Akisoma hotuba kwa
niaba ya waziri mkuu –Waziri wa sera bunge,
kazi, vijana, ajira, na wenye ulemavu Jenista Mhagama anasema, “pamoja na
uchanga wa sekta ya mifuko ya jamii nchini, mifuko hiyo kufanikiwa mpaka
kufikia kuwa na mifuko saba ya hifadhi ya jamii nchini, ambapo imefanikiwa kuwa
na wanachama wapatao 2.1 milioni na michango yenye thamani ya shilingi 1.9
trilioni”.
Hata hivyo waziri
Mhagama ametoa wito kwa waajiri wote nchini kuboresha mazingira ya kazi yawe
salama kwa wafanyakazi pamoja na kulipa michango yao kwa wakati.
Vilevile katika
kuhakikisha zana ya “HAPA KAZI TU” inafanya kazi waziri Mhagama aliongeza kwa
kusema “…ni
lazima tutambue waotufanyia kazi ni binadamu na hakuna binadamu aijuaye kesho. Hivyo
changieni mfuko huu kwa moyo mmoja sio tu kwa sababu ni hitajio la serikali,
bali pia kama motisha kwa wafanyakazi”.
Kutokana na mfuko wa
fidia kwa wafanyakazi (WCF) kuwa mchanga na kujulikana kwa wananchi wengi,waziri
ameishauri bodi ya kutumia vyombo vya
habari na mitandao ya kijamii kuwafikishia ujumbe na matarajio yay a mfuko huu
kwa wafanyakazi na waajiri.
Lakini pia ameongeza
katika kutekeleza majukumu vizuri, WCF inahitaji madaktari wenye weledi wa
kubainisha magonjwa yatokanayo na ajali kazini, hivyo kuweka mpango endelevu wa
namna ya kuwaainisha, kuwawezesha na kuwajengea uwezo.
Post a Comment