Askari wa jeshi la DRC wakiwa wamembeba mzobemzobe mmoja wa raia aliyekuwa akiandamana kupinga kuendelea kwa Rais Kabila madarakani.
|
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo Joseph Kabila. |
Askari wa jeshi la kongo
wakiwazuia raia waliokuwa kwenye maandamano mjini Kinshasa.
HABARI KWA UNDANI
|
Wakati muhula wa pili na wa mwisho kwa ukiwa umekamilika tarehe 19
Disemba, kumekuwa na maandamano katika miji kadhaa nchini Congo na miji mingine
duniani ya kumtaka rais wa DR Congo Joseph Kabila kujiuzulu na leo ni siku ya
mwisho ya utawala wake, lakini uchaguzi umeahirishwa ambapo upinzani wanasema
kuwa ni jaribio la Kabila kusalia madarakani.
Muungano wa vuguvugu la kidemokrasia ulizindua
kampeni ya ''Bye-Bye Kabila'' ili kumshinikiza kung'atuka muhula wake
unapokamilika mwezi Disemba.
Kulingana na mtandao
wa Politico
unasema takribani watu watatu walikuwa wanasemekana kuuawa na wanajeshi mjini Kinshasa na wengine watano
walijeruhiwa, wawili vibaya baada ya kupigwa
risasi wakiwa karibu na maofisa wa kikosi cha Republican Guard katika mojawapo ya wilaya
zenye idadi kubwa ya watu wa N'djili.
Wananchi wamekuwa
wakiimba Kabila Must Go –‘kabila ni sharti aondoke’ huku milio ya risasi ikiendelea
kusikika kwenye maeneo tofauti mjini Kinshasa, licha ya kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi ametaka kufanyika kwa
maandamano ya Amani ambayo yamekuwa yakifanyika katika miji kadhaa ya DR Congo.
Post a Comment