MAREKANI.
Wanachama wapatao 538 wa jopo maalum la kumchagua rais nchini Marekani wanakutana Jumatatu hii katika miji mkuu ya majimbo yote hamsini ili kumteua atakayemrithi rais Barack Obama kama rais wa Marekani.
Taarifa zinasema mgombea ni lazima apate wingi wa kura za wajumbe ama kura 270 za wajumbe 538 ili kushinda urais.
Kuna takriban wajumbe 538.Wengi wao ni maafisa waliochaguliwa au viongozi wa vyama, lakini majina yao hayapo katika makaratasi ya kupigia kura na pia hawajulikani na umma.
Mamilioni ya raia wa Marekani ambao wanamuona Donald Trump kama asiyeweza kuongoza Marekani, wametia sahihi ombi katika mtandao wakiwataka wajumbe wa Republican kuzuia uchaguzi wake.
Hata hivyo wajumbe wapatao 37 watalazimika kufanya hivyo ili kumzuia kuchaguliwa kuwa rais.
Kambi ya Republican imepinga hatua hiyo ikisema ni jaribio la wanachama wa Democrat wasiotaka kukubali kushindwa na imelalamika kwamba baadhi ya wajumbe wamenyanyaswa kufuatia kura hiyo muhimu.
Moja ya jopo linalomuidhinisha kwa kura rais wa Marekani. |
Japokuwa maamuzi hayo ni ya kawaida nchini Marekani kufuatia matokeo kama hayo kwa uchaguzi wa mwaka 2000 ambayo George Bush alimshinda mpinzani wake Al Gore, matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu uliojaa wasiwasi yaliwashangaza wengi pale.
Historia inaonyesha kwamba sio jambo la kawaida kwa mjumbe kukaidi matakwa ya wapiga kura wa jimbo lake, huku baadhi wakiwa wameenda kinyume na matakwa hayo, hawajaweza kubadili msimamo wao kuhusu mtu atakayechukua ikulu ya White House kwa muhula wa miaka minne.
Post a Comment