0

UGANDA:
Maofisa kadhaa wa polisi wa kiume nchini Uganda walivalia viatu vya kike na kushiriki katika matembezi yenye lengo la kuhamasisha jamii dhidi ya udhalilishaji na dhuluma dhidi ya wanawake nchini humo.

Polisi hao walikuwa wanashiriki katika matembezi yanayofahamika kama Tembea Maili Moja na Kiatu Chake ('Walk A Mile in Her Shoes') Polisi hao waliandaa matembezi hayo kwa ushirikiano na mashirika ya kutetea haki za wanawake.

Shirika hilo la Walk A Mile in Her Shoes linaloandaa matembezi hayo lilianzishwa mwaka 2001 na Frank Baird, lilianza kama kundi la wanawake waliokuwa wakijitokeza na kutembea kwenye bustani wakiwa wamevalia viatu vya wanawake.
Lakini sasa limekuwa shirika kubwa na kila mwaka maelfu ya watu hushiriki kuchangisha pesa za kusaidia vituo vinavyowasaidia waathiriwa wa ubakaji, pamoja na wale waliothiriwa wa dhuluma majumbani pamoja na miradi inayokabiliana au kupinga dhuluma na unyanyasaji wa wanawake, lengo likiwa ni kumpa nafasi mwanamke awe na nafasi na haki.

Post a Comment

 
Top