Mfanyabiashara maarufu barani Afrika Aliko Dangote. |
DAR ES SALAAM:
Hatimaye mgogoro
uliosababisha kusimamishwa kwa uzalishaji katika kiwanda cha saruji cha
Dangote, kilichopo mkoani Mtwara , inaelekea umekwisha baada ya tajiri bilionea
Mnigeria Aliko Dangote kukutana na Rais John Pombe Magufuli hapo jana jijini
Dar es Salaam.
Katika
mazungumzo hayo, Rais Magufuli amemhakikishia mfanyabiashara huyo kuwa serikali
ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wote nchini kwa
lengo la kuimarisha sekta ya viwanda nchini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko. |
HABARI KWA UNDANI: Baada ya mazungumzo hayo Rais Magufuli na mwekezaji huyo
walijitokeza kwa waandishi wa habari katika viwanja vya Ikulu mjini Dar es
salaam na wote kuhakikisha kuwa matatizo yote yaliyosababisha kusimama kwa
uzalishaji yameshughulikiwa.
Rais Magufuli alisema watu
aliowaita “walipiga
dili” ndio walioingilia shughuli za biashara na kusababisha kukwama
kwa uzalishaji. Dangote alihakikisha kuwa bado ana nia ya dhati ya kuwekeza
Tanzania na kwamba anataka kununua mali zote ghafi za kiwanda hicho ndani ya
Tanzania.
Pia
amekanusha uvumi unaondelea kuhusu kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote
akisema kuwa hakukuwepo na tatizo lolote ila watu waliotaka kujinufaisha binafsi
kupitia mradi huo
Amemtaka Dangote kununua gesi
moja kwa moja kutoka TPDC ambacho ni chombo cha serikali badala ya kutumia watu
ambao wamekuwa na nia ya kutengeneza faida tu.
Mvutano kati ya serikali
ya na kampuni ya Dangote ilijitokeza
mwanzoni mwa mwezi Disemba baada ya kampuni hiyo kutangaza kusimamisha kwa muda
uzalishaji wa saruji katika kiwanda hicho chenye thamani ya dola za Marekani milioni 600, ambacho tangu kuzinduliwa kwake bei ya saruji nchini imeshuka kwa zaidi ya asilimia 30.
Kiwanda
cha Dangote ambacho kina uwekezaji mkubwa katika sekta ya uzalishaji saruji
kuliko viwanda vingine vyote vilivyopo Afrika Mashariki kina uwezo wa kuzalisha
saruji takriban tani milioni tatu kwa mwaka na kimetoa ajira ya moja kwa moja
kwa zaidi ya watu 1,000 mkoani Mtwara.
Post a Comment