Maisha yana changamoto
zake, visa na mikasa vinaambatana na maisha ikiwa ni sehemu yake, hapo kale
hukujua siri ya maisha mpaka pale ulipopatwa na jambo lililokupelekea
kujifunza, hebu jifunze zaidi kupitia kisa hiki.
Mama mmoja aliuguliwa
ghafla na mtoto wake majira ya usiku yapata saa 2, mtoto alibanwa na kifua
(asthma), hali ilikuwa mbaya na mama akaenda kuomba msaada kwa jirani yake
aliyekuwa na gari, lakini jirani akamjibu gari haina mafuta, akaenda kwa
mchungaji ili amsaidie, akajibiwa nina wachungaji toka Marekani, hivyo sitaweza
kuwaacha peke yao.
Mama hakuwa na jinsi
aliamua kumbeba mtoto ili amuwahishe hospitali akiwa na hofu asije kufa kama
baba yake aliyefariki miaka michache kwa ugonjwa huo.
HARI YA KUOGOFYA:
Kulikuwa na kichaa mmoja
mchafu aliyekuwa akizungukazunguka mitaani na jalalani alipomuona yule mama
anavyohangaika na mtoto akamwendea na kumchukua mtoto bila kuongea na mama wa
mtoto, kisha akamweka begani, mama hakuwa na la kusema ila kumwelekeza
Hospitali, yule kichaa alielewa akaenda haraka hadi Hospitali.
Alipofika madaktari
walipomuona yule kichaa na mtoto wakajua kuna dharura, wakamchukua mtoto na
kumhudumia kwa haraka, baada ya dk10 yule mama wa mtoto akawasili, kisha
madaktari wakatoa taarifa kuwa endapo mtoto angecheleweshwa kwa dakika 5
angekufa.
Mungu alimtumia yule
kichaa mchafu kuokoa maisha ya mtoto. Hivyo usimteegemee Mchungaji Jirani wenye
magari, matajiri nk. Mungu huweza kuinua mtu usiyemdhania kukubariki. Mwamini
Mungu atakubariki.
Usimtumaini mwanadamu
hakuna baraka kwake. Mungu huinua vinyonge ili kuangusha vyenye nguvu.
Kupitia ujumbe huu unaweza
kuwashirikisha marafiki ili kupata kuona nguvu za Mungu zinavyofanya kazi.
-Mhariri habari.
.
Picha zilizopo katika kisa hiki hazina uhusiano wowote wala uhusika.
Post a Comment