![]() |
| Ulinzi wakati wa tukio hilo uliimalishwa |
MALTA:
Ndege ya serikali ya Libya -
Afriqiyah Airways iliyokuwa inasafiri kutoka Sebha kusini magharibi mwa Libya
ikielekea Tripoli safari ambayo kwa kawaida inachukua zaidi ya saa mbili, ilitekwa
nyara na kuelekezwa katika kisiwa kidogo cha Malta kilichoko katika bahari ya
Mediterranean, ambacho ni mwanachama wa Jumuiya ya Ulaya, kipo kilomita
takriban 500 kaskazini mwa Tripoli.
Waziri
mkuu wa Malta, Joseph Muscat amesema kupitia akaunti yake ya Twitter Ijumaa
kwamba watekaji nyara wa ndege ya Libya wamejisalimisha kwa vyombo vya dola, amesema watekaji hao walishuka kutoka kwenye
ndege na wahudumu walibakia ndani yake.
Ndege
hiyo ilielekezwa Malta, kilomita 500 kaskazini mwa pwani ya Libya baada moja wa
watekaji nyara kuwaambia wahudumu kuwa wanalo bomu la mkononi. Ndege hiyo
ilikuwa kwenye safari zake za kawaida nchini Libya.
![]() |
| Abilia wakishuka katika ndege hiyo. |
Awali,
abiria hao walishuka chini na mabasi yaliletwa ndani ya uwanja kuwaondoa hapo.
Picha za televisheni hazikuonyesha ishara zozote za mapambano au ving’ora na taarifa
za awali zimesema mmoja wa watekaji nyara aliwaambia wahudumu kuwa yeye ni
“mfuasi wa Gaddafi”
Lakini
pia haikuwekwa bayana ni kitu gani watekaji hao walikuwa wanataka. Kiongozi
huyo wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi aliuwawa katika machafuko ya mwaka
2011, na nchi hiyo ikaingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Afisa
wa juu wa Usalama wa Libya ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba
Ijumaa asubuhi wakati ndege iko safarini rubani aliwafahamisha kitengo cha
mawasiliano ya anga katika uwanja wa ndege wa Mitiga kuwa ndege imetekwa nyara.
“Rubani aliripoti kwa waendesha
mawasiliano mjini Tripoli kwamba walikuwa wametekwa, na baada ya hapo
wakapoteza mawasiliano,” afisa huyo alisema akiombwa asitajwe jina. “Rubani huyo alifanya bidii kujaribu
kuwashawishi watue katika uwanja wa ndege kwa salama lakini walikataa.”
Moja ya tukio kubwa la
utekaji nchini Malta lilitokea mwaka 1985, pale ambapo wapalestina walipoiteka
ndege ya Egyptair. Makamando wa Misri waliivamia ndege na baadhi ya watu
waliuwawa.


Post a Comment