0
DAR ES SALAAM.
Tafiti zimekuwa zikitolewa zikiwa na lengo na kuonyesha utafiti ulipoegemea kuwa na nini ndani yake, hivi karibuni umefanyika utafiti unaoonyesha kuwa, mwananchi mmoja kati ya watano yaani asilimia 22; ana akaunti benki yake mwenyewe au ya ushirika na mtu mwingine.utafiti huo unaosema  hili ni ongezeko la asilimia 19 tofauti na mwaka 2014.


Miongoni mwa wale wasio na akaunti benki (asilimia 78), nane kati ya kumi wanataja kutokuwa na fedha kama sababu kuu ya kutokuwa na akaunti benki. Umiliki wa akaunti za benki unatofautiana katika ya makundi mbalimbali: kaya tajiri asilimia 56; kaya masikini asilimia 6; wananchi wa mjini asilimia 41; wananchi wa vijijini asilimia 13; wanaume asilimia 24, na wanawake asilimia 20.

Matokeo haya yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,800 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara (Zanzibar haihusiki kwenye matokeo haya) kati ya tarehe 14 na 26 septemba 2016, utafiti huu ulitolewa na Twaweza ni  takwimu kutoka Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mikononi.

Mkurugenzi mtendaji wa Twaweza, Ndugu Aidan Eyakuze
“Upatikanaji wa huduma rasmi za kifedha kumeongezeka kwa kiwango kikubwa nchini. Upatikanaji na uwezo wa kutuma na kupokea pesa kwa urahisi na usalama, na sehemu salama za kuweka akiba yoyote vinasaidia kupunguza ugumu wa maisha ya watu masikini na kuongeza uzalishaji wao.  Wakati huo huo, huduma rasmi za kifedha kwa sasa zinashikiliwa kwa kiwango kikubwa na mitandao ya simu za mikononi. Na takwimu zinaonyesha kuwa huduma hizi hutumika kwa kiasi kikubwa kutuma na kupokea fedha. Hii inamaanisha kuwa wananchi wengi hawafurahii ongezeko la huduma ikiwemo bima, upatikanaji wa mikopo na akiba. Ni wajibu wa makampuni ya mitandao ya simu za mikononi, benki na taasisi nyingine za kifedha kufanya kazi kwa pamoja na kutoa huduma zitakazowasaidia wale ambao hawajafikiwa na huduma hizi muhimu.” Alisema mkurugenzi mtendaji wa Twaweza, Ndugu Aidan Eyakuze. 


Hali hii imepelekea serikari kujiwekea lengo jipya la kufikia asilimia 80 ifikapo mwaka 2017. Kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania idadi ya watanzania waliokuwa wamefikiwa na huduma na kifedha kupitia simu za mkononi ilikuwa asilimia 50 mwaka 2014 hivyo basi utafiti huu wa Sauti za Wananchi umeonesha kwamba kuongezeka kwa idadi ya waliofikiwa na huduma hizi ni dalili njema.

Hata hivyo ifahamike kuwa wahojiwa wa Sauti za Wananchi hupewa simu za mkononi ili kufanikisha zoezi la kupata takwimu sahihi zisizo na ubaguzi, inaonyesha  kuwa upatikanaji wa huduma nyingine za kifedha pia umekua nchini Tanzania, ingawa ni kwa kiwango kidogo ukilinganisha na huduma za fedha kwenye mitandao ya simu za mikononi.

Post a Comment

 
Top