Moshi mkubwa unaotokana na moto unaounguza
mabasi yaliyokuwa tayari kuwaamisha raia.
|
SYRIA.
Wakati dunia ikiwa inatafuta Amani kwa watu kuishi
pasi kuwepo madhara au balaza kuu la usalama la umoja wa Mataifa likiwa ndiyo
lenye jukumu la kuangalia Amani na kulinda raia duniani, Mabasi kadhaa
yaliokuwa yakielekea kuwaokoa wagonjwa na watu waliojeruhiwa katika kijiji
kinachomilikiwa na serikali katika mkoa wa Idlib nchini Syria yamechomwa na
waasi, Msafara
huo ulikuwa ukielekea Foah na Kefraya maeneo yaliozungukwa na waasi.
Maelfu na maelfu ya wasyria wenye hofu na waasi waliokwama
huko wamekua wakisubiri zowezi la kuwahamisha, mapema Jumapili iliyopita msemaji
wa ICRC Elodie Schindler, aliwapa matumaini raia hao aliposema,"kamati
yetu iko tayari kuanza tena kazi ya kuwaondosha watu kutoka Aleppo mashariki
kuanzia asubuhi ya leo".
Raia wa Syria akiendesha pikipiki huku akipita karibu
na moja ya mabasi yaliyochomwa moto na waasi.
|
Kupitia shirika la habari la Syria SANA, liliripoti kwamba mabasi ya
kuwahamisha wakazi wa Aleppo yanayosimamiwa na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba
Mwekundu, ICRC, yameingia katika mitaa ya mji huo uloharibiwa kutokana na vita
Jumapili asubuhi kuanza kazi ya kuwahamisha wakazi walobaki.
Mpango wa awali wa kuwasafirisha watu mashariki mwa mji wa Aleppo
haukufanikiwa kwa siku ya Ijumaa, ambapo uliwaacha raia wakiwa wamekwama katika
vituo tofauti bila chakula, maji na makazi ambapo maelfu ya watu wanatarajia
kuondoka katika eneo hilo.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajia kupiga
kura Jumapili mchana ikiwa itawapeleka wafuatiliaji kwenye mji huo mkubwa wa
Syria uloharibika kufutilia zoezi la kuwahamisha watu pamoja na kuwasaidia kwa
kuwapatia ulinzi raia walobaki.
Pia litazungumzia muswada
wenye azimio na uliotayalishwa na Ufaranasa unaoeleza kuzorota kwa mzozo wa kibinadamu ndani na karibu ya mji
huo na uwezekano wa maelfu ya wakazi wa Aleppo wanaohitaji msaada na kuondolewa
katika mji huo.
Post a Comment