MWANZA.
Taifa lolote duniani
linahitaji watu wenye elimu ili kufikia matarajio yanayoweza kupatikana
kutokana na upana wa mawazo unaotokana na wasomi waliopo kwa wakati huo, ili
kuendelea huwezi kuepuka kuwa na watu waliofunguka akili kupitia upana wa
mawazo yaliopatikana kutokana na elimu.
Chuo kikuu cha
mtakatifu Augustino ni moja kati ya vyuo vikuu nchini vinavyosimamiwa na kanisa
katoliki na kutoa elimu ya juu kwa wananchi wa kada tofauti na uwezo tofauti. Kwa
mujibu wa Makamu mkuu wa chuo hicho Fr. Thadeus Mkamwa anasema, kilianzishwa kutokana
na serikali kutoa nafasi watu binafsi kuwekeza katika sekta hii ya elimu ya
juu.
Katika hotuba yake
kwenye mahafari ya 18 yaliobeba ujumbe “Changia katika mchango wa SAUT kuandaa na kutoa wahitimu
bora na mahiri kwa jamii” chuoni hapo, Fr. Mkamwa anasema ” katika dunia ya
sasa hakuna chuo chochote duniani kunachomuandaa mwanafunzi katika ukamilifu
bila mchango kutoka kwa wadau mbalimbali, kama serikali, watu binafsi,
mashirika ya umma, viwanda, ndugu au marafiki, katika kutambua hilo tunaomba
wadau watuunge mkono katika kuandaa kwa pamoja kozi na program ambazo jamii,
viwanda, mashirika vinahitaji.”
Kupitia mahafali yam
waka huu wahitimu wapatao 2652 wa fani mbalimbali wamepewa vyeti, kwa kuzingatia
utoaji wa elimu bora na yenye tija chuo hicho kimejiwekea mipango endelevu ya
kuwaendeleza wahadhiri na wafanyakazi kitaaluma ili kwenda sambamba na utoaji
wa huduma za kitaalamna utafiti kwa nyanja mbalimbali iki kuweza kuchochea
maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
Kwa upande mwingine
amezungumzia taarifa za serikali ya vyuo vikuu vya Afrika mashariki yam waka 2014
iliyosema kuwepo kwa upungufu wa wahandisi na wataalam wa fani mbalimbali
wanaowez kuvuna na kutunza rasilimali kadhalika upungufu wa wajuzi wenye uwezo wa kuvuta wateja/wanunuzi, ripoti hiyo
inatahadhalisha hadi kufikia 2025 asilimia 93 ya kazi zote nchini zitahitaji
usomi na ujuzi wa ziada wa elimu ya sekondari.
“kupunguza umasikini ni pamoja na
kupunguza idadi ya wajinga katika nchi,nimesema wajinga, siyo wapumbavu kwa
sababu haitafika siku ambayo Tanzania itasema hatuhitaji tena wasomi, kwa kuwa
tumejitosheleza kielimu, elimu haina mwisho, hivyi tujitahidi kujenga misingi
ya elimu na siyo kubomoa elimu yetu” alisema Fr. Thadeus
Mkamwa.
Katika hatua nyingine
iliyoibua maswali kwa baadhi ya wahitimu ni pale alipozungumzia suala la mikopo
kwa baadhi ya wahitimu wanaotoka katika familia masikini kuwa wasipewe mikopo,
hapa alijikita katika Bodi ya mikopo nchini na kusema, “tunaishauri serikali kutafuta njia
mbadala kwa ajili ya kunusuru vijana hususani kutoka familia masikini na
fukara, wanafunzi hawa wamekuwa kero vyuoni, wanakuja bila ada wakitegemea pesa
ya mikopo ya ada, malazi na chakula, wanafunzi wanatoa lawama kwa vyuo kana
kwamba vyuo vina wajibu wa kuwasubiri mpaka wapate pesa.”
Aitha katika kutoa
suruhisho ni ni kifanyike kutokana na kila mtu ana haki ya kupata elimu
ikizingatia mfumo wetu wa elimu umewekwa katika kuwasaidia wanafunzi wa elimu
ya juu kupewa mikopo na kulipa baadaye anasema, “mikopo wapewe wanafunzi wanaotoka katika
familia zinazoweza kulipa kwani wanakopesheka, bali kwa wanafunzi masikini wao
wapewe misaada, grants au scholarships ilimradi wawe wametimiza vigezo. Huwezi kuwapa
mkopo watu masikini ambao hawawezi hata kulipa ada kidogo,masikini hakopesheki
iwe mtu au nchi, unamkopesha masikini halafu unafukuzana naye ili akulipe, huo
siyo uchumi.
Kwa upande wa uhakiki
unaoendelea ameitaka serikali kufanya uhakiki huo kwa usawa wote na vigezo sawa
na isiwe kwa chuo hiki unahakiki na kile unakiacha.
Post a Comment