0
DAR ES SALAAM.
Serikali imesema itayafanyia uchunguzi madai yaliyoripotiwa na vyombo vya habari vya Malawi jana madai ya wapelelezi nane kutoka Tanzania walikamatwa wakati wakijaribu kinyume cha sheria kuingia mgodi kwenye urani katika nchi hiyo.



Taarifa za kukamatwa kwa mara ya kwanza zilichapishwa Alhamisi iliyopita, na vyombo vya habari wa Malawi jana vilipendekeza kuwa walikuwa wapelelezi nane  waliotumwa na serikali ya Tanzania pasipo kuwa na vitambulisho vya kusafiria kuchunguza kama nchi hiyo "inaendeleza silaha za nyuklia kutoka machimbo ya uranium Kayerekera eneo lililoko wilaya ya Karonga.


Dr. Augustine Maige.

Waziri wa mabo ya nje, afrika mashariki na Ushirikiano wa kimataifa, Dk Augustine Mahiga, alisema kuwa hajui chochote kuhusiana na ripoti hiyo ilahidi kufuatiliaji, "Mimi ndiyo kwanza nasikia taarifa hii kwa mara ya kwanza kutoka kwako. Haya ni madai makubwa, nitayafanyia kazi na kuwasiliana na ubalozi wetu huko malawi kuona kama wanajua chochote kuhusu hili …"alisema Dk Mahiga.

Vyombo vya habari wa Malawi vimenukuliwa pasipo kutaja majina kwa usalama kuwa baadhi ya waliokamatwa walikuwa na vifaa, pamoja na kamera nzito.



Naibu msemaji wa jeshi la polisi eneo la karonga nchini malawi, Bw George Mlewa alisema "Wakati uchunguzi wetu unaendelea juu ya suala hilo, naweza kukuambia kwamba hatuna taarifa hizo hadi sasa”.


Polisi walisema wanakijiji katika kijiji cha Kayuni nchini Malawi walishangaa kuona Watanzania wakitembea kuzunguka na walipowahoji na kuwauliza kwa wanafanya nini kwenye mgodi, walishindwa kutoa majibu ya kushawishi, alisema Bw Mlewa na kuongeza huu ni wakati tuhuma maana wanakijiji waliwaita polisi, ambao kwa haraka wakaja na kukamatwa wageni hao nane


Source: Malawian medias and Citizen

Post a Comment

 
Top