Matukio katika picha mbalimbali 20 pamoja na habari kwa undani ambapo wananchi wa Kenya waishio nchini Tanzania waliposherehekea siku
kubwa ya uhuru wa nchi yao wakiongozwa
na balozi wa kenya nchini Tanzania.
=====================================
Kunapokuwa
na sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa inaambatana na kukata keki, hii ndiyo keki
iliyoandaliwa rasmi kwa wananchi wa Kenya kula kuashilia miaka 53 ya Uhuru wa
Taifa lao.
|
Balozi wa kenya Mwakweru kulia na Balozi Maiga
kushoto wakipeana mikono baada ya tukio la kukata keki.
|
Mshauli
wa balozi kenya Peter K. Sang kulia akiteta jambo na Jean Uku Afisa mauzo wa
shirika la ndege la Precision Air katika hafla hiyo.
|
Balozi
wa Kenya Mh. Chiray Mwakweru (kulia) na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano
wa kimataifa na kikanda Balozi Maiga (kulia) wakiongea mambo kadhaa.
|
Katikati
ni mshauri wa ubalozi wa Kenya Peter Sang, (kushoto) Waziri –Balozi Maiga na (wa pili kulia)
Balozi wa Kenya nchini mh. Mwakweru.
|
Picha
ya pamoja balozi wa kenya Mh. Chiray Mwakweru (wa sita kutoka kulia) akiwa na
baadhi ya maofisa wa Ubalozi wa Kenya nchi pamoja naye waziri wa mambo ya nje
Balozi Maiga (katikati)
|
HABARI KWA UNDANI:
DAR ES SALAAM:
Sehemu ya Uhuru wa
maisha ya mtu anayetoka katika kutokuwa chini ya imaya ya mtu mwingine na
nafasi ya kufanya mambo yake kwa kutumia nafasi binafsi pasipo kubugudhiwa wala
kuwa chini ya utawala ni hatua ya kuwa huru.
Nchi ya kenya
imesherehekea miaka 53 ya uhuru wa nchi yake toka itoke mikononi mwa mkoloni
mwingereza hivyo basi wananchi kukumbuka madhira na hatua walizopitia mpaka kufikia
mwaka huu 2016 ambapo ni hatua ndefu iliyopitia ikiwa ni milima na mabonde.
Katika salamu zake kwa
wakenya waishio nchini, maafisa wa balozi kadhaa waliohudhulia sherehe hizo,
balozi wa kenya nchini Mh. Chiray Ali Mwakweru ameelezea hatua ambazo serikali
ya Kenya imepiga toka pale walipopata uhuru kuwa ni hatua ambazo zinaungwa
mkono na wakenya wote, hata Rais wa sasa Uhuru Kenyatta anapigania maendeleo
hayo kutokana na jitihada anazofanya katika kuliinua taifa hilo zaidi ya hapo.
Pia aliongeza kwa
kuweka ucheshi’ kuhusiana na maendeleo ambayo wakenya wamepiga pamoja na wao
kuwa nyuma kupata uhuru, lakini wamekuwa wa kwanza kutumia huduma ya kutuma
pesa kwa kutumia simu ya kiganjani maarufu kama mpesa. Lakini hakuacha kuwataja
makamanda wa kudai uhuru katika nchi ya Tanzania na Kenya Nyerere na Kenyatta.
Kwa upande wake waziri
wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa na kikanda wa Tanzania Balozi Augustine
Maige amekumbuka mwaka 1963 alipokuwa Iringa mara alisikia mara kadhaa Redio
Tanzania wakati huo ikipiga nyimbo zilizokuwa zinaisifu kenya.
Aliongeza kuwa, ndipo
alipogundua kuwa kuna kitu kimetokea na wakenya wamepata uhuru, pamoja na pongeza
mafanikio yaliyopatikana bado anaona ushirikiano wa nchi za afrika mashariki
uliohasisiwa na viongozi wawili unatakiwa kupewa nafasi kwa kizazi kipya
kujifunza na kugundua mambo mengi ambayo kwa sasa hayapatikani.
Pia wakati juhudi za
Rais Magufuri za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda basi kuna kila haja ya
wakenya kuja kuwekeza na kutumia fulsa iliyopo sasa ili kuendana na falsafa za
viongozi wakuu wa nchi hizi.
Post a Comment