Antonio
Guterres akiapishwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa Jumatatu ya 12/12/2016
HABARI KWA UNDANI:
MAREKANI:
Jumatatu hii alipatikana
katibu mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa akitokea nchini Ureno Antonio Guterres ambapo
anakuwa katibu mkuu wa 9 ambapo aliapishwa siku hiyo na kuwa kuanza kuitumikia
taasisi hiyo inayosimamia uwanja mpana ikiwemo Amani, kuepusha na kuingilia
mambo kadhaa yanayoweza kuleta madhara kwa binadamu nk.
Wakati akihutubia mataifa
wanachama makao makuu ya umoja huo, Guterres alisema Umoja wa Mataifa lazima
uwe wenye kutekeleza majukumu yake kwa wakati, na kuongeza Umoja huo lazima pia
uangazie maswala yanayohusu watu kabla ya kuzingatia zaidi mikakati.
Kiongozi huyo mwenye umri wa
miaka 67 na aliewahi kuwa waziri mkuu 1995- 2002 na pia kiongozi wa shirika la
kushughulikia wakimbizi la Umoja wa Mataifa kuanzia mwaka 2005- 2015, alishinda
wagombea wenzake zaidi ya 12 kwenye mchujo wa uchaguzi uliochukua miezi 10.
Hata
hivyo bwana Gueterres anakabiliana na kibarua kigumu wakatidunia ikishuhudia
tatizo la uhamiaji, mapigano kwenye ukanda wa mashariki ya kati na Afrika,
ugaidi, mabadiliko ya hali ya hewa, pindi atakapochukua rasmi kiti hicho mwezi
Januari mosi kutoka kwa katibu mkuu wa Umoja huo anaeondoka Ban Ki –moon.
|
Post a Comment