Ephraim Kwesigabo mkurugenzi wa Sensa ya Watu na
Takwimu za Jamii (kulia) na Mtakwimu Mkuu
(Pricipal Statistics) Muhidin Mtindo
|
Pamoja na kukosekana
kwa mvua na upatikanaji wa bidhaa muhimu kama chakula na bidhaa nyingine
kumekuwapo na tatizo la kupanda na kushuka kwa bidhaa mbalimbali hapa nchini
hali inayochangia baadhi ya wananchi kukosa kuwa na bajeti katika maisha ya
kila siku.
Ofisi ya Taifa ya
Takwimu imetoa taarifa za mfumuko wa bei Taifa kwa mwezi uliopita wa Novemba mwaka
huu ambapo umeongezeka mpaka kufikia asilimia 4.8 kutoka 4.5 kwa mwezi Octoba
mwaka huu. Kutokana na hali hiyo kasi ya upandaji wa bidhaa na huduma kwa mwaka
huu 2016 imeongezeka ikilinganishwa na mwaka uliopita 2015.
Katika upigaji wa
hesabu uliofanywa kuonyesha mfumuko huo wa bei, haukuweza kujumuisha vyakula
vinavyoliwa nyumba na kwenye migahawa, vinywaji baridi, dizeli, petrol, gesi ya
kupikia, mkaa, umeme, kuni na mafuta ya taa,
Pamoja na hayo Ephraim Kwesigabo amesema, mfumuko wa
bei kwa mwezi novemba 2016 umeongezeka kwa asilimia 1.1 ikilinganishwa na
ongezeko la 0.1 kwa mwezi uliopita, ambapo bei za vyakula na bidhaa zisizo vya
vyakula zilizochangia kuongezeka ni pamoja na mbogamboga asilimia 7.4, unga wa
ngano 2.4, unga wa muhogo 1.7 unga wa mahindi 1.5, mtama 1.5, dagaa wakavu 1.1,
mchele 1.0.
Hata hivyo uwezo wa shilingi ya Tanzania katika
kununua bidhaa na huduma zilezile za mlaji umeongezeka kwa senti 12. Ikilinganisha
na mwezi octoba 2015 kutoka shilingi 95.86 mpaka shilingi 95.98 kwa mwezi
novemba 2016.
Hali kadhalika mfumuko wa bei kwa nchi ukanda wa
Afrika Mashariki bado unashabihiana, nchini kenya mfumuko wa bei umepanda kwa
asilimia 6.68 kutoka asilimia 6.42 kwa mwezi octoba 2016 na nchini Uganda
mfumuko umeongezeka kutoka asilimia 4.6 kutoka asilimia 4.1kwa mwezi octoba
2016.
Hivyo basi hapa nchini umepanda kutoka 4.5 mpaka
4.8.
Post a Comment