Mazingira unayoishi yanafaa kukupa nafasi kufanya mazoezi |
Mazoezi ya nusu saa mara tatu kwa wiki kwa wanaume
yana uwezo wa kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mbegu za kiume kwa mujibu wa
wanasayansi, wanaume
ambao wameendelea na zoezi la kukimbia kila wakati, mbegu zao huwa na afya
njema, kulingana na watafiti wa jarida la maswala ya uzazi.
Watafiti
wamesema ni muhimu kufanya mazoezi hayo kwa kiwango cha wastani, kwa sababu
mazoezi ya kupita kiasi hudhuru kiwango cha uzalishaji wa mbegu hizo za kiume,
utafiti umebaini kwamba wale wanaoshiriki katika michezo kama vile ya
uendeshaji baiskeli wanauwezo wa kupunguza kiwango cha mbegu zao za uzazi.
Hizi ni mbinu chache za
kuongeza mbegu za kiume:
§
Weka korodani katika madhari mazuri, kwa kuepuka kuvalia suari
za ndani za kukaza.
§
Usioge na maji moto sana.
§
Epuka magonjwa ya zinaa.
§
Wacha uvutaji wa sigara.
§
Punguza kiwango cha pombe.
§
Usinone sana.
§
Fanya mazoezi, lakini kwa kiwango cha wastani.
|
TAFITI: Wanaume wapatao 261 waliosajiliwa katika majaribio
hayo hawakuwa na matatizo yoyote ya kiafya au shida ya uzazi. Walikuwa na
kiwango sawa cha bengu za uzazi na zilizokuwa na afya, na walioishi maisha bila
kufanya mazoezi.
Wanaume hao walishirikishwa kwenye mradi mmoja kati ya miradi minne ikiwemo:
§
Kutofanya mazoezi
§
Mazoezi makali mara tatu kwa wiki (dakika moja ya mbio ya kasi
na mapumizo mafupi katika kila dakika kumi)
§
Mazoezi wa wastani mara tatu kwa wiki ( dakika 30 katika mashine
ya kufanyia mazoezi)
§
Mazoezi makali , mara tatu kwa wiki( kwa karibu saa moja katika
mashine ya kufanyia mazoezi)
Mafunzo ya mazoezi yalionekana kuongeza kiwango cha mbegu za uzazi
zilizo na afya. Pia
yalionekana kuongeza kiwango cha mbegu za uzazi zilizo na afya huku waliofanya
mazoezi yaliowastani walipata matokeo bora zaidi.
Wanaume
wote katika makundi matatu walipunguza uzani wao na walipata matokeo bora
ikilinganishwa na wanaume ambao hawakufanya mazoezi kwa wiki 24 katika kipindi
cha majaribio.
Muda unapaswa kupangwa ili kufanya mazoezi |
Mafunzo ya mazoezi yalionekana kuongeza kiwango cha mbegu za uzazi
zilizo na afya. Pia
yalionekana kuongeza kiwango cha mbegu za uzazi zilizo na afya huku waliofanya
mazoezi yaliowastani walipata matokeo bora zaidi.
Wanaume
wote katika makundi matatu walipunguza uzani wao na walipata matokeo bora
ikilinganishwa na wanaume ambao hawakufanya mazoezi kwa wiki 24 katika kipindi
cha majaribio.
Watafiti
wamesema manufaa waliopata wanaume hao ni kutokana na kupunguza uzani katika
makundi matatu, wote walipunguza kiwango cha mafuta kutoka kwa miili yao. Tayari
wamebaini kwamba unene kupita kiasi unaweza kusababisha shida za uzazi. Robo
tatu ya wanaume hao walikuwa na uzani kupita kiasi.
Huduma ya kwanza ya kuimarisha mbegu za
uzazi ni gani?
Shida za uzazi kwa wanaume zinaweza kuwa kubwa na iwapo wanaume wataweza kubadili njia zao za kuishi zinaweza kukabiliana na shida hizo kwa urahisi. Kwa mujibu wa Prof. Allan Pacey wa chuo kikuu cha Sheffield.
Mtafiti
mkuu Behzad Hajizadeh Maleki amesema, “kulingana na
matokeo hayo yamebaini kwamba kufanya mazoezi inaweza kuwa mbinu rahisi, na
bora ya kuimarisha mbegu hizo za uzazi kwa wanaume ambao wanachangamoto za
uzazi.” Alikiri bayana kwamba wanaume wengine hawapati watoto si kwa
sababu ya ukosefu wa viwango vya mbegu zao za kiume.
Kile kitu ambacho hakijajulikana ni iwapo mazoezi huchangia kuimarisha mbegu za uzazi. Hili ni jambo ambalo watafiti wanahitajika kuchunguza zaidi kwenye mahabara kuchunguza iwapo mazoezi huchangia katika ongezeko la mbegu za uzazi.
Nchi ya Uingereza imewasihi watu wazima kufanya mazoezi kwa dakika 150 kama vile kuendesha baiskeli, au kutembea kwa haraka, ama dakika 75 ya mazoezi yanayotumia nguvu kama vile kukimbia kila wiki.
Post a Comment