Miss Andrea Pusic kutoka
Marekani
|
Kwa miaka kadhaa
duniani kina mama na watoto wamekuwa ni wahanga wakubwa kutokana na madhara
yatokanayo eidha kutokana na vita, majanga ya moto, matatizo ya kifamilia hata
ajali za barabarani au magonjwa yanayoweza kumfanya kudhulika na kupata kilema
katika mwili.
Kufuatia hali hiyo
chama cha madaktali bingwa wa nchini Marekani wakishirikiana na wenzao wa
Tanzania kutoka hospitali ya Taifa ya
Muhimbili na Aga Khan wanaendesha zoezi la kufanya uchunguzi kwa kinamama na
watoto ili kuweza kubaini athali walizo nazo na kufikia hatua ya kufanya
upasuaji.
Moja ya upasuaji
unaotarajia kufanywa ni yale yanayoweza kuonekana kwa nje, ili kumfanya
mwanamke au mtoto aliyeathirika kutokana na majanga hayo kumrudishia viungo
vilivyoathirika kuweza kufanya kazi vizuri.
Wakati zoezi hili
likiwa ni muendelezo wa zoezi lililowahi kufanyika januari mwaka jana
lililojulikana kwama women for women, huku vyombo vya habari vikiwa ni sehemu
kubwa katika kuwapata waathirika wa matatizo haya, wiki hii linafanyika zoezi
la upasuaji mdogo kwa watu 15 na upasuaji mkubwa kwa watu 25.
Habari zaidi inapatikana hapa chini:
Post a Comment