Dr. John Pombe Magufuri |
DAR ES SALAAM:
Mkutano
mkuu wa Chama cha Mapinduzi ulioketi jijini Dar Es Salaam umefanyika huku
ukionyesha muelekeo mpya kwa wanachama wa chama hicho huku kukiwa na
marekebisho ya kupunguza idadi ya wajumbe wa vikao vya chama hicho.
Katika uchaguzi
huo ambao umekwenda tofauti na baadhi ya mitizamo/utabiri wa baadhi ya watu
umemrudisha kitini katibu mkuu wa sasa Abdulhman Kinana huku majina ambayo hayakupewa
nafasi ndugu Rodrick Mpogolo na Humphrey Polepole yakiingia kuchukua nafasi za utendaji katika
chama hicho kikongwe cha siasa nchini.
Humphrey Polepole |
Katika hatua nyingine baadhi wa idadi ya wajumbe wa chama hicho iliyokuwa inafikia 388 na kupunguza mpaka kufikia 158 huku kamati kuu iliyokuwa na watu 34 sasa itakuwa na watu 24.
Wakati Humphrey
Polepole akichukua nafasi ya katibu mwenezi, Rodrick Mpogolo yeye anakuwa naibu katibu ccm bara hali hii inaonyesha nafasi ya
Mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuri ya kuwa timu ndogo ya watenda kazi itakayoendana na
kauli mbiu yake ya hapa kazi tu, huku uhakiki wa wanachama wa chama hicho ukiwa
upo njiani.
Post a Comment